JAMHURI YA MUUNGANO
YA TANZANIA

WIZARA YA FEDHA
TANGAZO KWA UMMA
Katika siku za hivi karibuni, baadhi ya magazeti
yamekuwa yakitoa taarifa za upotoshaji juu ya suala la kuongezeka kwa malipo ya
pensheni kwa Waheshimiwa Wabunge.
Magazeti hayo yanadai kwamba Mheshimiwa Waziri wa Fedha amethibitisha
ongezeko hili. Taarifa hizo ziliendelea
kudai kwamba Waheshimiwa Wabunge watakapostaafu watastahili kulipwa shilingi
160 milioni kila mmoja.
Kwa kupitia tangazo hili, tunaeleza
kwamba, Mheshimiwa Waziri wa Fedha
hajawahi kuongea na Mwandishi wa Habari yeyote kuhusu suala la nyongeza ya pensheni
ya Waheshimiwa Wabunge na maelezo kwamba Mheshimiwa Waziri alithibitisha
taarifa za ongezeko hilo sio kweli
bali ni maelezo binafsi ya Waandishi wa Habari hizo na suala hilo halipo
Serikalini wala Bungeni.
Aidha, tunapenda
kuwaasa Waandishi wa Habari kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao na kuacha kuwachonganisha
Wabunge na Wananchi wanaowaongoza kwa kuwapotosha kwa masuala ambayo hayana
ukweli na uthibitisho wowote.
KATIBU MKUU – WIZARA YA FEDHA
5 FEBRUARI, 2014

No comments:
Post a Comment