Maafannde
wa Jeshi la Magereza Prison ya Mbeya jana jioni imeendeleza ubabe wa
kushinda mechi za mzunguko wa pili wa Ligi ya Vodacom kwa kuwabugiza
maafanbde wenzao timu ya JKT Ruvu mabao 6-0.Mchezo
huo ambao ulipigwa katika dimba la Sokoine huku huku ukihudhuriwa na
watazamaji wachache na mvua ikinyensha na kutotesha uwanja huo ulitoa
fursa kwa timu ya Prison kufanya vyema katika uwanja wake wa nyumbani.Katika
mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo Timu ya JKT Ruvu iliwachabanga Maafande
wa Prison mabao 3-1 hali ambayo ilisababisha mashabiki kuja juu na
kusababisha aliyekuwa kocha wa timu hiyo Jumanne Chale kutimuliwa katika
timu hiyo.
Prison
ikiwa chini ya kocha wake David Mwamwaja walianza kuhesabu karamu hiyo
ya magoli dakika ya 20 na Omega Seme ambapo alipiga shuti hafifu
lililomkuta golikipa wa JKT Ruvu Shaaban Dihile aliyeudaka na kumponyoka
na kisha kutinga wavuni.
Goli
la pili lilifungwa na Nurdin Choma dakika ya 29 baada ya piga nikupige
katika lango la JKT ambapo dakika 34 mchezaji wa Prison Lugano Mwangama
aliipatia timu yake goli la tatu kwa shuti iliyopigwa kutokea upande wa
kushoto na kumuacha golikipa Dihile akichupa bila mafanikio na mpira
kutinga wavuni.
Karamu
ya magoli katika kipindi cha kwanza ilihitimishwa dakika ya 44 ambapo
mchezaji wa timu ya Prison Peter Michael aliipatia timu yake goli la nne
alilofunga kwa kichwa.
Kipindi
cha pili kilianza kwa timu ya JKT Ruvu kufanya mabadiliko ambapo
golikipa Dihile alipumzika na nafasi yake kuchukuliwa na Sadikc Maksi.
Hata
hivyo mabadiliko hayo hayakuweeza kuisaidi timu ya JKT Ruvu ambapo
golikipa Maksi alionekana kung'aa dakika chache za mwanzo wa kipindi cha
pili na baadaye dakika ya 70 mchezaji wa timu ya Prison aliiandikia
timu yake bao la tano lililotokana na shuti kali iliyomuacha kipa Maksi
akichupa golini bila mafanikio.
Baada
ya kuingia kwa goli hilo kocha msaidizi wa timu ya JKT Ruvu Nelson
Haule alifanya mnabadiliko mengine kwa kumtoa mchezaji Amos Magisa na
kumuingiza Karage Mgunda, hata hivyo hakukuwa na mafanikio yoyote kwa
timu hiyo ambapo wachezaji wa JKT RUVU walionekana kushindwa kuutawala
mchezo kutokana na kuteleza uwanjani na kuanguka kila walipolikaribia
lango la timu ya Prison.
Karamu
ya magoli kwa siku ya leo ilihitimishwa na mchezaji Peter Michael
ambaye alifunga bao la 6 dakika ya 82 baada ya mashambulizi yaliyotokea
katika lango la JKT lililosababisha wachezaji wa timu hiyo kupoteana na
kumfanya Michael apate fursa ya kufunga bao hilo kiurahisi.
Hadi
kipenga cha mwisho kinapulizwa Prison ilitoka kifua mbele kwa mabao 6-0
ambapo katika hatua nyingine ubao wa magoli katika uwanja huo ulisomeka
magoli 5 1-0 kutokana na kile kilichoelezwa kuwa hakukuwa na ubao wa
magoli zaidi ya 6 katika uwanja huo wa Kumbukumbu ya Sokoine.
NA MKWIDA BLOG
No comments:
Post a Comment