Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, February 20, 2014

RIVALDO MIAKA 41 ACHEZA MECHI PAMOJA NA MWANAWE MWENYE MIAKA 18

rivaldo d2e7d
MSHINDI wa Kombe la Dunia na gwiji wa Brazil, Rivaldo ameweka historia baada ya kuonyesha picha akiwa na mwanawe uwanjani anayetumia jina la baba yaje huyo.
Rivaldo, mwenye umri wa miaka 41, aliingia uwanjani akitokea benchi wakati Mogi Mirim wakitoa sare ya 1-1 na XV de Piracicaba katike mechi ya ligi ya jimbo la Sao Paolo Uwanja wa Romildo Ferreira.
Ilikuwa mara ya kwanza anacheza sambamba na mwanawe huyo mwenye umri wa miaka 18, Rivaldo Junior.
Kinda Rivaldinho ana safari ndefu kama kweli anataka kufuata nyayo za baba yake, aliyejipatia umaarufu mkubwa kwenye soka.
Katika mataji, Rivaldo ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia maarufu kama Ballon D'Or mwaka 1999 katikati ya miaka yake mitano ya kuichezea Barcelona ambayo alishinda mataji ya UEFA Super Cup, mawili ya La Liga na Kombe la Mfalme.
Aliiongoza Brazil kutwaa Kombe la Dunia mwaka 2002 kabla ya kwenda kuongeza taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na vigogo wa Italia, AC Milan.
Rivaldo, ambaye pia amechezea Santa Cruz, Corinthians, Palmeiras, Deportivo La Coruna, Cruzeiro, Olympiacos, AEK Athens, Bunyodkor, Sao Paulo, Kabuscorp na Sao Caetano, alirejea kwa mara ya pili Mogi Mirim Desemba mwaka jana ambako aliibukia kisoka. Pia ni rais wa klabu hiyo kwa sasa. Chanzo: binzubeiry


No comments:

Post a Comment