Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu, akisalimiana na makamishna wa
Jeshi la Polisi baada ya kuwasili kwa ajili ya kumpokea mgeni rasmi
Naibu Waziri wa Mambo ya ndani kwenye ufunguzi wa mkutano Mkuu wa
Maofisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika katika chuo cha
taaluma ya Polisi Moshi.
Naibu
waziri wa Mambo ya Ndani Mh, Pereira Ame Silima akisalimiana na Mkuu wa
Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu baada ya kuwasili katika Chuo cha
Taaluma ya Polisi Moshi kwa ajili ya kufungua mkutano Mkuu wa Maofisa
wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika katika chuo hicho.
Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akitoa hotuba jana katika ukumbi
wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi
kufungua mkutano Mkuu wa Maofisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi
unaofanyika katika chuo hicho.
No comments:
Post a Comment