Kilimanjaro
Tanzania Music Awards (KTMA2014),
ni tuzo ambazo hufanyika kila mwaka kwa lengo la kutambua kazi bora za
wasanii ambazo zimefanya vizuri ndani ya mwaka mzima. Mapema hii leo,
Meneja wa bia ya Kilimanjaro, Bwana George Kavishe alifungua tuzo hizo
rasmi na kutoa maelezo kwa mabadiliko ambayo yamejitokeza mwaka huu…
Baadhi ya mabadiliko ambayo yataonekana safari hii, ni kwa mara ya
kwanza mashabiki watakuwa na nafasi ya kupendekeza kwa njia ya SMS,
barua pepe na kupitia tovuti jina la msanii, kikundi au mtayarishaji wa
Muziki aliefanya vizuri.
Pia, kwenye tuzo za mwaka huu, vipengele vitakavyopigiwa kura vitakuwa 34.
No comments:
Post a Comment