
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye akizungumza na wageni waalikwa kwenye sherehe za Usiku wa Wasanii
na Waandishi wa Habari zilizofanyika usiku wa tarehe 2 Februari kwenye
ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Mbeya.

Mbunge wa Mbinga Magharibi Kapteni John
Komba akizungumza na waandishi wa habari na wasanii wa muziki na sanaa
za filamu Tanzania kwenye siku ya Usiku wa Wasanii na Waandishi wa
Habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Mbeya, katika
usiku huo Komba alisisitiza wasanii kuangalia maisha yao ya mbele na sio
sasa kwani wasipojiandaa wataaibika hapa ulimwenguni pia alisisitiza
juu ya maslahi ya wasanii kuongezwa kutokana na kazi kubwa wanazofanya
na thamani ya kazi wayofanya.

Wasanii wakimpongeza Kapteni John Komba kwa wosia mzuri aliotoa juu yao .

Msanii Maarufu nchini Hafsa Kizinja akitumbuiza siku ya usiku wa Wasanii na Waandishi wa Habari,Februari 2 mjini Mbeya ,siku ambayo CCM ilisheherekea miaka 37 ya kuzaliwa kwake na kitaifa sherehe hizo zilifanyika mjini hapo.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbali
mbali wakijumuika kumshangilia Mwenyekiti wao wa Kikosi cha Ziara
mkongwe Richard Mwaikenda akijimwaga wakati wa sherehe za Usiku wa
Wasanii na Waandishi wa Habari zilizofanyika tarehe 2 Februari siku
ambayo CCM ilisheherekea ktutimiza miaka 37 ya kuzaliwa kwake na sherehe
kufanyika kitaifa mkoani Mbeya.

Wasanii wa tasnia ya Filamu wakiwa wamepozi kwenye sherehe za usiku wa Wasanii na Waandishi

Msanii wa Siku Nyingi nchini Dokii
akisalimiana na Mwigulu Lameck Nchemba Naibu Waziri Wizara ya Fedha
(Sera) wakati wa sherehe za usiku wa Wasanii na waandishi wa Habari.

Baadhi ya waandishi kutoka Jjiji la
Mbeya wakipata vinywaji na maongezi kidogo wakati wa sherehe fupi za
kukutana pamoja na waandishi na wasanii wa muziki na filamu
zilizofanyika tarehe 2 Februari mjini Mbeya.

Waandishi wa Umoja wa Waandishi wa
Habari mkoani Mbeya wakizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana wakati wa sherehe fupi za kupongezana kwa kazi nzuri wakati wa
maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM lakini pia usiku huo ulipewa
jina la Usiku wa Wasanii na Waandishi wa Habari.

Wasanii wakongwe wa tasnia ya filamu Tanzania nao walikuwepo kutoka kushoto ni Baba Haji, JB na Rich.

Kila mtu maarufu alikuwepo kwenye tasnia ya sanaa za maigizo na filamu.

Malkia wa Taarab nchini Hadija Kopa akitoa vionjo vya nyimbo yake mpya ambacho kinasema hata Obama anamjua.

Katibu wa NEC Itikadi na Unenezi wa CCM
Nape Nnauye akiimba sambamba na band ya TOT wakati wa usiku uliopewa
jina la usiku wa Wasanii na Waandishi wa habari.

No comments:
Post a Comment