Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, March 6, 2014

Ajali yaua saba, 11 hoi

 
Watu saba wamekufa na wengine 11 kujeruhiwa baada ya basi la dogo aina ya Nissan Civilian walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori katika barabara kuu ya Chalinze- Segera wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
 
Watu saba wamekufa na wengine 11 kujeruhiwa baada ya basi la dogo aina ya Nissan Civilian walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori katika barabara kuu ya Chalinze- Segera wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei, ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia jana katika eneo cha Chalinze Mzee jirani na kwamba majeruhi tisa kati yao ni mbaya.

Kamanda Matei alisema basi hilo lenye namba za usajili T573 CQD likitokea Msata kwenda jijini Dar es Salaam liligongana na lori hilo lenye namba T921 BFD/T 470 BFY wakati likitoka Chalinze kuelekea Tanga.

Kamanda Matei aliwataja waliokufa kuwa ni Dege Ally, Tunu Said Khalfan, Tumaini Hussein, Jafar Suleiman, Emmanuel David na wawili ambao   majina yao hayajafahamika.

Kadhalika, Kamanda Matei aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni dereva wa basi hilo, Ndege Ally, kondakta wake, Deo Mosses, Bitela Msuha, Zaina Mkombozi, Salumu Idd na Chadugu Paulo.

Wengine ni Abdul Wela ambaye ni mwanafunzi darasa la kwanza shule ya Kwaifugo Mkata, Geoffrey Anthony, Juma Athuman, Shaban Omar  ambaye ni dereva wa lori na Shoshy Mohamed ambaye ni utingo wake na majeruhi wengine bado majina yao hayajatambulika.

Kwa mujibu wa Kamanda Matei, majeruhi wengi wa ajali hiyo wameumia vibaya sehemu za miili yao na wapo waliovunjika miguu na mikono na wote kupelekwa Kituo cha Afya Chalinze kupatiwa matibabu.

Kamanda huyo ambaye alifika katika eneo la tukio muda mfupi baada ya ajali hiyo, alisema kuwa chanzo chake hakijajulikana na kwamba uchunguzi unaendelea.

Mganga Mkuu wa Kituo hicho, Dk. Victor Bamba alisema kuwa wakati ajali hiyo ikitokea, watu watano walikufa papo hapo na wengine 13 kujeruhiwa.

Dk. Bamba alisema wakati wakikimbizwa kwenye kituo hicho cha afya mmoja  alifia njiani na mwingine kituoni hapo wakati akipatiwa matibabu.

Alisema watu hao wawili waliokufa walikuwa miongoni mwa majeruhi tisa waliokuwa mahututi kutokana na kujeruhiwa vibaya baada ya ajali hiyo kutokea.

Alisema majeruhi waliosalia walihamishiwa walihamishiwa katika hospitali Teule ya Mkoa wa Pwani ya Tumbi iliyopo wilayani Kibaha.

NIPASHE lilipofika Tumbi, mwandishi hakuruhusiwa kuingia wodini kwa maelezo kwamba ni lazima aruhusiwe na Ofisa Habari, Gelard Chami, ambaye hata hivyo alikuwa kwenye kikao.

Baadaye Chami akizungumza kwa simu jioni alithibitisha kupokelewa kwa majeruhi hao kati ya hao usiku wa manane jana.

Alisema kati ya hao, sita walipatiwa matibabu na kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo na wengine wanaendelea na matibabu kutokana na hali zao kuwa mbaya.Chami alisema kuwa wawili kati ya hao wanatarajia kufanyiwa upasuaji mkubwa.

MASHUHUDA

Hata hivyo, kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, Hussein Halfan na Yusufu Hussein, ajali hiyo ilitokana na uzembe wa dereva wa Nissan kwani ilikuwa ikiongozana na Toyota Hiace na ilipofika eneo hilo, Hiace ilitoka upande wa kulia wa barabara na kuyapita malori waliyokuwa mbele yake na dereva wa Nissan aliifuata Hiace bila kusubiri lori lililokuwa mbele na hivyo kukutana nalo uso kwa uso.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment