Jana
katika gazeti hili tulichapisha habari iliyokuwa ikielezea kuwa Rais
Jakaya Kikwete aliwatembea wagonjwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na
Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (MOI) jijini Dar es Salaam.
Katika habari hiyo tuliwataja aliowatembelea kuwajulia hali kuwa ni Rajab Maranda, ambaye anatumikia kifungo cha miaka 18 jela kwa wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), pamoja na mwandishi wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Salum Mkambala.

Hata
hivyo, taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais
imeeleza kuwa Rais Kikwete hakwenda kumuona Maranda bali aliwatembelea
wanahabari wawili ambao ni Salum Mkambala wa Channel Ten aliyelazwa wodi
binafsi D, na Margaret Chambiri wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi aliyelazwa
wodi binafsi .
Taarifa hiyo pia inaeleza kuwa Rais Kikwete aliwajulia hali wagonjwa wengine wawili, John Mhina na Reuben Nyanga ambao wako chumba kimoja na Mkambala.
Tunachukua nafasi hii kuomba radhi kwa Rais Kikwete kwa usumbufu ambao ameupata kutokana na habari hiyo.
CHANZO: Mwananchi.

No comments:
Post a Comment