Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka (kushoto),
akimsikiliza Mkuu wa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT), Dkt. Zakaria
Mganilwa ofisini kwake kabla ya kupokea magari mawili ambayo
yamekabidhiwa kwa chuo hicho na Shirika la Transaid la nchini Uingereza,
hafla ya kukabidhi magari hayo imefanyika leo asubuhi katika viwanja
vya NIT.
(Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi
Taswira ya tanker trailer la futi 40 na Folk Lift ambayo
yamekabidhiwa kwa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) na Kampuni ya
Transaid leo asubuhi katika viwanja vya chuo hicho. Magari hayo
yatasaidia wanafunzi wanaosoma kozi za udereva chuoni hapo.
Sehemu
ya Wafanyakazi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), wakimsikiliza
Mgeni Rasmi (hayupo pichani), wakati wa hafla fupi ya kukabidhi magari
mawili kwa ajili ya kufundishia mafunzo ya udereva chuoni hapo, magari
hayo yalimekabidhiwa leo asubuhi na Shirika la Transaid la nchini
Uingereza.
Mkurugenzi
wa Mradi ya Usalama Barabarani wa Shirika la Transaid la Nchini
Uingereza, Mr. Neil Rettie (mwenye tai ya blue) akimkabidhi funguo za
gari aina ya Iveco kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban
Mwinjaka kwa ajili ya mafunzo ya Udereva yanayotolewa na Chuo Cha Taifa
Cha Usafirhsaji (NIT), Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya chuo
hicho leo Asubuhi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka akiwasha gari ya kuinulia mizigo focal liftkama
ishara ya kupokea moja ya magari mawili yaliyokabidhiwa na Shirika la
Transaid la nchini Uingereza kwa Chuo cha Taifa cha Usafirshaji (NIT),
leo asubuhi. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji
(NIT), Dkt. Zakaria Mganilwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban Mwinjaka, akiwasha gari aina ya Folk Liftlililokabidhiwa
kwa Chuo Cha Taifa Cha Usarifshaji (NIT), kwa ajili ya wanafunzi
wataochukua mafunzo ya udereva chuoni hapo. Magari hayo yamekabidhiwa
leo asubuhi katika viwanja vya Chuo hicho.
No comments:
Post a Comment