ASILIMIA 40 ya Wanaume waliopima vinasaba ili kubaini uhusiano wa kibaiolojia
na watoto wanaowalea, wamebainika kuwa watoto hao si wao licha ya kuzaliwa na
wake zao au wapenzi wao.
Taarifa hiyo imetolewa na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kutokana na wanaume
waliotaka kufahamu ukweli kuhusu watoto wao hadi Januari mwaka huu kwa mujibu
wa Sheria ya Vinasaba vya Binadamu namba 8 ya mwaka 2009.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Usimamizi na Udhibiti
wa Kemikali za Viwandani na Majumbani, kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali,
Sabanitho Mtega, bado kuna tatizo la wanaume wengi kubebeshwa mzigo wa kuwalea
watoto ambao si halali yao, licha ya kuaminishwa na wenzao wao kuwa ni damu
yao.
Mtega, ametoa taarifa hiyo kwenye mahojiano na
waandishi wa habari jijini Mbeya wakati wa Warsha ya siku Moja ya kuwaelimisha
Wateja wa huduma za Mkemia Mkuu wa Serikali, lakini pembezoni mwa warsha hiyo,
wanaume wanaona ni bora kulea mtoto bila ya k upima DNA kwani hatua hiyo ni
hatari kwa uimara wa ndoa zao.
Hata hivyo, Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai
mkoani Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Robert Mayala, amesema vipimo hivyo
vimesaidia kutatua kesi nyingi za kubaini uhusiano baina ya baba na mtoto.
Warsha hiyo imewahusisha Waingizaji, Mawakala,
Wasafirishaji, Wauzaji na Watumiaji wa kemikali na wadau wengine wa sekta hiyo
wakiwemo TRA, Jeshi la Polisi, Madaktari na Waandishi wa Habari.
DC NYAMWESE:KITUO CHA KUPOOZA UMEME HANDENI KULETA MAPINDUZI YA UWEKEZAJI
-
*Na Mwandishi Wetu*
*Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Salum Nyamwese, ameridhishwa na kasi ya
utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kituo cha kupooza umeme (sub...
6 hours ago


No comments:
Post a Comment