Mahakama ya Umoja wa Mataifa inyoshughulikia Mauaji ya Halaiki ya Rwanda (UN-ICTR) iliyo na makao yake makuu mjini Arusha leo imetoa msaada wa magari mawili ya kiusalama (Amoured Cars) kwa jeshi la polisi mkoani Arusha ili kuimarisha shughuli zake za kiusalama mkoani hapo. Magari hayo ni baadhi ya yale yliyokuwa yakitumika kwa shughuli za usalama - kubebea watuhumiwa au watu nyeti - na mahakama hiyo inyotarajiwa kumalisha shughuli zake mwakani. Magari hayo ni yale yaliyoimarishwa kiusalama ambapo hata risasi haziwezi kupenya kwenye bodi yake au kwenye kioo chake. Magari hayo yalikabidhiwa na Mkuu wa Idara ya Fedha na Kaimu Mkuu wa Utawala wa Mahakama hiyo Bw. Robert Foot kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo Afande Liberatus Sabas
DC NYAMWESE:KITUO CHA KUPOOZA UMEME HANDENI KULETA MAPINDUZI YA UWEKEZAJI
-
*Na Mwandishi Wetu*
*Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Salum Nyamwese, ameridhishwa na kasi ya
utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kituo cha kupooza umeme (sub...
4 hours ago

No comments:
Post a Comment