
Mgomo wa wahudumu wa magari nchini Kenya
Huduma
za usafiri jijini Nairobi zimekwama kufuatia hatua za wenye magari
kugoma hii leo wakilalamikia nyongeza ya ada ya kuegesha magari jijini
humo.
Maelfu
ya wafanyakazi wamelazimika kutembea kwa miguu na wasafiri wa kutoka
jijini kwenda maeneo ya mashambani nao kulazimika kuahirisha safari zao.
Mwenyekiti
wa wenye matatu katika eneo la Mlima Kenya, Bwana Michael Kariuki,
ambaye aliongea na BBC akiwa nje ya lango la kuingia kwenye afisi ya
Gavana wa Kaunti ya Nairobi, alisema mzozo uliopo ni mdogo na waweza
kusuluhishwa haraka.
"Juzi
tulikuwa na Gavana Evans Kidero na tukakubaliana kiasi tunachopaswa
kulipa lakini jana tulipofika wafanyakazi wa kaunti wakakataa kiasi
tulichokuwa nacho," Bwana Kariuki alisema.

Wahudumu wa magari ya umma wakigoma Nairobi
Jiji
la Nairobi ni mojawapo wa kaunti ambazo zimebuniwa chini ya Katiba
iliyopitishwa na wapiga kura na kuidhinishwa mwaka 2010 katika hatua ya
kuimarisha huduma kwa wananchi.
Kaunti
hizo mpya hata hivyo zimejikuta njia panda baada ya kupata madaraka
bila fedha za kuandamana nayo; ambapo zimelazimika kuongeza kodi kama
njia mojawapo ya kujiimarisha kiuchumi.
Mkuu
wa polisi nchini Kenya, David Kimaiya aliagiza idara ya trafiki nchini
Kenya kunasa magari yote yaliyofunga barabara za mji.

Maafisa wa polisi wakingoa nambari za usajili za magari ya umma yaliyogoma
mjini Nairobi.Chanzo BBC Swahili

No comments:
Post a Comment