Mamlaka
za kipolisi jijini New York, zimethibitisha kuwa watu wawili wamepoteza
maisha ndani ya moja ya nyumba vilivyokuwa katika jengo moja la ghorofa
ambalo limeanguka leo hii.
Vituo vya habari katika eneo hilo vimetoa ripoti zenye kueleza pia kuwa
kuna watu wapatao 11 ambao wameonekana kuwa na majeraha kadhaa kutokana
na tukio hilo ambalo wenyeji wa maeneo hayo wameeleza kuwa limetokana
na kitu kama mlipuko.
"Taarifa toka kwa wenyeji wa eneo hili zinaonyesha kuwa kulisikika kitu
kama mlipuko kwanza katika mtaa huu wa 116, kabla ya jengo kuanza
kuporomoka" ameeleza msemaji mmoja wa serikali jijini hapo.
Safari za treni katika eneo hilo zilisitishwa mara moja, huku pia
vikosi vya usalama vikiliweka eneo hilo chini ya karantini huku takriban
wafanyakazi 168 wa kwenye vituo vya nishati vilivyo katika maeneo ya
jirani wakiwa wameondolewa katika maeneo yao ya kazi.
Aidha, kampuni moja ya kutoa huduma za kusambaza gesi katika maeneo
hayo, imeamuriwa kufunga huduma zake haraka iwezekanavyo, ili kuepusha
majanga zaidi hii ikitokana na ukweli kuwa, kulisikika mlipuko mkubwa
toka katika moja ya vyumba kwenye jengo hilo.
Raia mmoja ameeleza kuwa, amekuwa akisikia harufu ya gesi kila
alipopita mahali hapo, kwa takriban wiki moja kabla ya tukio hili.
"Tuliona watu wakirushwa kutokea madirishani, hawa walikuwa majirani
zangu, na kwa ujumla kishindo kilikuwa kikubwa sana kama bomu vile, na
kilitetemesha jengo zima" ameeleza shuhuda mmoja, ambaye aliungwa mkono
na shuhuda mwingine alyesema hali haikuwa tofauti na ilivyokuwa wakati
wa tukio la kulipuliwa kwa majengo pacha kwenye sakata la September 11
No comments:
Post a Comment