Mtangazaji wa Channel Salumu Mkambala, akipelekwa Theatre katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha, Pwani.
Msanii
wa kundi la Mizengwe, Hemed Maliyaga (wa kwanza kulia) akisaidiana na
ndugu pamoja na mke wa Mkambala (wa tatu kushoto) kumpeleka mgonjwa
Theatre.
...Mkambala akiingizwa Theatre.
STORI: DEOGRATIUS MONGELA
Baada
ya Mtangazaji wa Channel Salumu Mkambala kupata ajali na kugongana na
lori akiwa safarini kuelekea Morogoro sababu za ajali hiyo zimetajwa.
Akizungumza
na mwandishi wetu Hospitali ya Tumbi Kibaha, Pwani mdogo wa
mtangazaji huyo, Ramadhani Mkambala alisema kaka yake alikuwa akielekea
Morogoro na alipofika maeneo ya Vigwaza aligongana na lori alfajiri saa
10. 30 akiwa yeye na mtu mmoja aliyempa lifti.
Hata
hivyo, chanzo cha ajali hiyo kilitajwa na Ramadhani kuwa ni kutokana na
barabara ya eneo hilo kuwa na mashimo mengi hali iliyosababisha gari la
kaka yake kuhama upande wake na kulivamia lori.
“Tulipopata
taarifa tulishtuka sana lakini tunashukuru Mungu kuona kaka yangu yupo
hai na amepata matibabu hapa Hospital ya Tumbi japokuwa ameumia mikononi
na miguu na kuwekewa bendeji ngumu (POP) lakini tuna matumaini atapona
na kuendelea na majukumu yake,” alisema Ramadhani.
HABARI KWA HISANI YA GPL
No comments:
Post a Comment