Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, March 3, 2014

MUFTI WA TANZANIA AENDA INDIA KWA MATIBABU

Sheikh Issa Bin Shaaban Simba.
Mufti wa Tanzania, Sheikh Issa Bin Shaaban Simba ameondoka nchini kuelekea India kwa ajili ya matibabu.
Aliongozana na ujumbe wa watu wawili, akiwemo Katibu Mkuu wa Baraza la WaislamU Tanzania(BAKWATA), Suleiman Lolila na Diwani wa Kata ya Kwadelo wilayani Kondoa, Omari Kaliati.
Kwa mujibu wa taarifa iliyomfikia mwandishi na kuthibitishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Bakwata anayeshughulikia Utawala,  Yusufu Yasini, Sheikh Simba aliondoka saa 10 jioni kwa kutumia ndege ya Shirika la Oman Air.
Mufti alifika uwanjani hapo na kuingia kupitia eneo la wageni mashuhuri (VIP) huku akisindikizwa na msafara wa pikipiki ya polisi. 
Naibu Katibu Mkuu wa Bakwata anayeshughulikia Dini, Mohammed Khamis aliahidi kutoa taarifa zaidi kwa mwandishi, kuhusiana na safari hiyo. 
Mara baada ya kutapa taarifa za safari hiyo juzi, mwandishi alimtafuta Naibu Katibu Mkuu Utawala wa Bakwata, aliyekiri Mufti kusafiri.
Hata hivyo, alishindwa kutoa taarifa kwa ufasaha, kwa madai kuwa hakuwa katika nafasi nzuri ya kuzungumzia suala hilo. 
"Sipo katika nafasi nzuri ya kuzungumzia suala hilo kwa kuwa nipo barabarani, naendesha gari, nitafute kesho (jana) nitaweza kukupa taarifa vizuri," alisema Yusufu.
Alipotafutwa tena jana kupitia simu yake ya mkononi, hakuweza kupatikana baada ya simu hiyo kuwa imezimwa.
Juhudi za kuwatafuta viongozi hao zinaendelea kufanywa na mwandishi ili kupata taarifa zaidi ya safari ya kiongozi huyo mkuu wa  Waislam nchini

No comments:

Post a Comment