JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
RPC.
Ofisi ya Kamanda wa
Polisi,
Mkoa wa
Mbeya,
Namba ya simu 2502572
S. L. P. 260,
Fax - +255252503734
MBEYA.
E-mail:- rpc.mbeya@tpf.go.tz
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 12.03.2014.
·
MWANAMKE MMOJA AMUUA MUME WAKE KWA KUMKATA NA
KITU CHENYE NCHA KALI KICHWANI.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIWA
WATU WANNE KWA KOSA LA KUFANYA BIASHARA BAADA YA MUDA KUISHA.
MWANAMKE MMOJA AMUUA MUME WAKE KWA KUMKATA NA KITU CHENYE NCHA KALI
KICHWANI.
MWANAMKE MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA
JINA LA ETINA SILUMBA (44) MKAZI WA
MPEMBA WILAYA YA MOMBA AMEMUUA MUME WAKE ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA MISHECK MWASHIUYA (52) MKAZI WA MPEMBA
WILAYA YA MOMBA KWA KUMKATA KISOGONI NA KICHWANI NA KITU KINACHODHANIWA KUWA NI
PANGA NA KISHA KUMVUNJA SHINGO NA MGUU WA KUSHOTO. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 10.03.2014 MAJIRA YA SAA 21:00 USIKU KATIKA KIJIJI CHA
IPAPA, KATA YA IPUNGA, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI. UCHUNGUZI UNAONYESHA
CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI WIVU WA KIMAPENZI. MTUHUMIWA KABLA YA KUTENDA TUKIO
HILO INADAIWA KULIKUWA NA UGOMVI KATI YAKE NA MAREHEMU. MTUHUMIWA AMEKAMATWA
KWA MAHOJIANO ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE. KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHAMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANDOA KUTATUA MIGOGORO YAO YA
KIMAPENZI KWA NJIA YA KUKAA MEZA MOJA YA MAZUNGUMZO BADALA YA KUAMUA
KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIWA WATU WANNE KWA KOSA LA
KUFANYA BIASHARA BAADA YA MUDA KUISHA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWASHIKILIA WATU WANNE WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. ULILE ERASTO (30)
2. ERNEST MJEMBE (40) 3. HAMIS MWANYOMBOLE (28) NA 4. HALIDI SAULI (33)
WOTE WAKAZI WA SOWETO JIJI NA MKOA WA MBEYA WAKIWA WANAFANYABIASHARA YA KUUZA
POMBE BAADA YA MUDA KUISHA. WATUHUMIWA
WALIKAMATWA MAJIRA YA SAA 01:15 USIKU
WA KUAMKIA TAREHE 12.03.2014 KATIKA
ENEO LA MAMA JOHN, KATA YA ILOMBA, TARAFA YA IYUNGA. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA
MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHAMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA KUFUATA NA KUZINGATIA TARATIBU ZA
KUENDESHA/KUFANYA BIASHARA ZAO ILI KUJIEPUSHA NA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment