Kama unakwenda kwenye Usaili au unahitaji kuonekana ni mtanashati eneo lako la kazi, namna ya uvaaji wako una matokeo makubwa wa jinsi watu wanavyokuchukulia na kukutizama. Katika kuvaa ni eneo ambalo kwa wanaume ni rahisi zaidi kuliko wanawake.
Kwa wanawake kuvaa au kuchagua mavazi ya kibiashara ni changamoto kubwa , si kwa mtizamo mbaya ila kwa kuonekana umevaa kibiashara zaidi.
Jaribu kujua uko katika nyanja ipi ya biashara na Mavazi yake
Inategemea unafanya Biashara katika mazingira gani, utaona mwajiri anavaa kawaida kuliko wengine. Ni vizuri kijifunza namna ya kuvaa katika kazi. Biashara na Mikutano kulingana na kanuni na taratibu za kazi. Kuna ofisi zinahitaji kuvaa kitanashati na kibiashara zaidi kuliko kawaida hivyo unahittaji kuwa na suti au magauni ya kikazi na yenye heshima au Suruari na Shati haina shida.
Onyesha Mwonekano wako Mzuri kwa Namna Unavyovaa
Ishu sio nguo uliyovaa bali umeivaaje? Makosa mengi yanayofanyika ni kuvaa vibaya hasa nguo zilizobana au nguo kubwa sana, hivyo nguo zinazobana sana zinakuonyesha maumbile ya ndani na kukufanya uonekane wewe ni zaidi ya kazi.
Ikiwa haujali namna unavyovaa inamaanisha hata mpangilio wa kazi zako hauujali vilevile. Hivyo uvaaji wako kazi unatakiwa uwe umepangiliwa kwa umakini, usivae ilimradi ni fasheni au nguo zenye rangi nyingi na vipodozi vingi. Lengo lako liwe kuonekana kikazi zaidi na mvuto
No comments:
Post a Comment