Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, March 15, 2014

Rais Kikwete kuhutubia bunge maalum wiki ijayo


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuhutubia bunge Maalum la KATIBA Kati ya Jumatatu na Jumanne wiki ijayo.
Mwenyekiti wa bunge Maalum la KATIBA Mheshimiwa Samuel Sitta ameliambia bunge Mara baada ya kuapishwa na kukabidhiwa kiti chake leo jioni.
Amesema kazi ya kuwaapisha wabunge wote iliyoanza leo jioni itakuwa ikifanyika hadi saa 3 usiku na kukamilika Jumapili.
Jumatatu wiki ijayo saa 10 jioni bunge hilo litakabidhiwa rasmi rasimu ya katiba na mwenyekiti wa bunge la Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba.
Mwenyekiti Sitta amemshukuru na kumpongeza aliyekuwa Mwenyekiti wa muda wa bunge Hilo Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho kwa ustahimilivu, busara, hekima NA uvumilivu aliouonyesha wakati akiliongoza bunge hilo kuandaa kanuni zake kwa kipindi cha wiki Tatu.
Amesema kazi ya kuandaa kanuni ilifanywa bila kanuni hivyo baadhi ya wabunge walitumia fursa hiyo kufanya vitendo visivyokubalika. 
Amewakumbusha wabunge kuwa kanuni zimepatikana NA hivyo wazifuate vinginevyo wasije wakamlaumu pale atakapochukua hatua kwa ukiukwaji aw kanuni hizo.
Akiwaaga wabunge aw bunge Hilo, Mheshimiwa Kificho amewaasa wabunge aw bunge Hilo kuwa na hekima, busara, subira NA hoja zenye mashiko wakati wakifanya kazi hiyo NA kuangalia zaidi maslahi ya taifa ili kuwapatia wananchi KATIBA ambayo haitawagawa bali itakayoimarisha umoja NA mshikamano wao.
Mheshimiwa Sitta na Makamu wake Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan wameapishwa leo jioni na Katibu wa Bunge la Katiba
Bw. Yahya Khamis Hamad aliyekuwa na Naibu wake Bw. Thomas Kashililla.
Imetolewa na
Idara ya Habari MAELEZO, Dodoma, 
Machi 14,2014

No comments:

Post a Comment