Add caption |
Na Boniface Wambura, TFF
Bodi ya
Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeifanyia marekebisho ratiba ya Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) ambapo sasa itamalizika Aprili 19 mwaka huu badala ya
Aprili 27 mwaka huu.
Marekebisho
hayo yamefanyika ili kutoa fursa kwa timu ya Taifa 9Taifa Stars)
kujiandaa kwa mechi za mchujo la Kombe la Afrika 2015 ambapo itacheza
raundi ya awali Mei mwaka huu.
Kutokana
na marekebisho hayo, Yanga itacheza na Prisons (Uwanja wa Taifa) Machi
26 mwaka huu katika mechi ya raundi ya 17 wakati Machi 19 mwaka huu
kwenye uwanja huo huo ni Yanga na Azam.
Machi 15
mwaka huu kutakuwa na mechi mbili; Azam na Coastal (Azam Complex), na
Mtibwa Sugar itacheza na Yanga (Jamhuri). Mgambo na Azam zitacheza Machi
26 mwaka huu Mkwakwani, na Aprili 9 mwaka huu Yanga itaialika Kagera
Sugar (Taifa).
Raundi ya
22 itaanza Machi 22 mwaka huu kwa mechi kati ya Kagera vs Prisons
(Kaitaba), JKT Ruvu vs Mbeya City (Azam Complex), na Rhino vs Yanga (Ali
Hassan Mwinyi). Machi 23 mwaka huu ni Simba vs Coastal (Taifa), Mgambo
vs Mtibwa (Mkwakwani), Ruvu Shooting vs Ashanti (Mabatini) na Azam vs
Oljoro (Azam Complex).
Machi 29
mwaka huu itaanza raundi ya 23 kwa mechi kati ya Ashanti vs Oljoro (Azam
Complex) wakati Machi 30 ni Mbeya City vs Prisons (Sokoine), Kagera vs
Ruvu Shooting (Kaitaba), Mtibwa vs Coastal (Manungu), JKT Ruvu vs Rhino
(Azam Complex), Azam vs Simba (Taifa), na Mgambo vs Yanga (Mkwakwani).
Raundi ya
24 inaanza Aprili 5 mwaka huu kwa Kagera vs Simba (Kaitaba), Ashanti vs
Mbeya City (Azam Complex). Aprili 6 mwaka huu ni Coastal vs Mgambo
(Mkwakwani), Oljoro vs Prisons (Sheikh Kaluta Amri Abeid), Rhino vs
Mtibwa (Ali Hassan Mwinyi), Ruvu Shooting vs Azam (Mabatini) na Yanga vs
JKT Ruvu (Taifa).
Aprili 12
mwaka huu inaanza raundi ya 25 kwa Mtibwa vs Ruvu Shooting (Mabatini),
Coastal vs JKT Ruvu (Mkwakwani), Prisons vs Rhino (Sokoine). Aprili 13
mwaka huu ni Mgambo vs Kagera (Mkwakwani), Simba vs Ashanti (Taifa),
Mbeya City vs Azam (Sokoine) na Oljoro vs Yanga (Sheikh Kaluta Amri
Abeid).
Raundi ya 26 ni Aprili 19 mwaka huu kwa Rhino vs Ruvu Shooting (Ali Hassan Mwinyi), Mbeya City vs Mgambo (Sokoine), Prisons vs Ashanti (Jamhuri, Morogoro), JKT Ruvu vs Azam (Azam Complex), Oljoro vs Mtibwa (Sheikh Kaluta Amri Abeid), Coastal vs Kagera (Mkwakwani) na Yanga vs Simba (Taifa)
No comments:
Post a Comment