Mkurugenzi
wa Kampuni ya Lino International Agency ambao ndio waandaaji wa
shindano la Redds Miss Tanzania, Hashim Lundenga akizungumza na mawakala
wa shindano hilo Dar es Salaam jana katika semina ya seku mbili.
Katikati ni Redd's Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa na Mshindi
wa pili, Latifa Mohamed. Shindano la Miss Tanzania linadhaminiwa na Kinywaji cha Redd's Original.
Baadhi
ya mawakala wa shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakiwa katika
semina ya siku mbili juu ya namna ya ufanyanyaji wa mashindano hayo
mwaka huu jijini Dar es Salaam jana. Shindano la Miss Tanzania
linadhaminiwa na Kinywaji cha Redd's Original.
======== ====== ====
MAWAKALA
wa mashindano ya urembo nchini wametakiwa kutafuta washiriki wenye
vigezo kwa ajili ya kushiriki michuano hiyo mwaka huu na hatimaye kupata
mshindi wa kitaifa “Redd’s Miss Tanzania 2014” atakayeipeperusha vyema
bendera ya Tanzania kwenye fainali za dunia.
Akizungumza
katika semina ya mawakala hao iliyofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya
Regency iliyoko Mikocheni jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Lino
Agency International, Hashim Lundenga, aliwataka kusaka washiriki bila
ya kuwanyanyapaa wasichana kutokana na maumbile yao.
Lundenga
alisema kuwa mawakala hawapaswi kutoa maamuzi ya washiriki wakati wa
mchakato wa kutafuta warembo na jukumu la kufanya hivyo litabaki kwa
majaji.
Mkurugenzi
huyo alisema pia mawakala wanaume wanatakiwa kuwa makini katika
mchakato huo wa awali na kuhakikisha wanaendeleza maadili ya Kitanzania
na kufanikisha sanaa hiyo inazidi kufanikiwa.
“Si
vizuri kuwakataa wasichana wanaotaka kushiriki kwa sababu eti wafupi au
sabau nyingine…kufanya hivyo si sahihi, pia huu ni wakati mwingine kwa
mawakala wanaume kuhakikisha mnavivuka viunzi kwa wasichana
wanaojiandaa kuwaweka mtegoni,” alisema Lundenga.
Aliwataka
mawakala hao pia kuhakikisha wanafanya mazungumzo na makampuni na
taasisi mbalimbali kwa ajili ya kusaka udhamini wa kufanikisha
mashindano yao ambayo yanaania ngazi ya vitongoji, wilaya, mikoa na
kanda.
“Kuhusiana
na zawadi pia mnatakiwa kuwa na makubaliano na washiriki kulingana na
uwezo wako wakala…hata kama uko tayari kutoa jiko waeleze hivyo,”
Lundenga aliongeza.
Aliwaeleza
pia mawakala hao kwamba mdhamini mkuu wa mashindano hayo ni Redd’s
Original ambayo imeahidi kutumia zaidi ya Sh. Milioni 500.
Happiness Watimanywa ndiye mrembo anayetetea taji la taifa na mshindi wa pili, Latifa Mohammed pia walikuwepo jana katika semina hiyo inayotarajiwa kumalizika leo
No comments:
Post a Comment