Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Sekretarieti ya Ajira,Riziki Abraham katika
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imekamata vyeti feki 1,035
(sawa na asilimia1.6) ya maombi ya kazi yaliyotumwa kwa miaka minne
tangu kuanzishwa kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza,
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Sekretarieti ya Ajira, Riziki Abraham,
alisema katika kupokea maombi ya kazi, wamebaini udanganyifu wa hali juu
wa vyeti kwa wanaomba kutoka makazini na wahitimu.
"Tangu
miaka minne iliyopita hadi sasa, Sekretarieti ya Ajira imebaini kuwapo
kwa matumizi ya vyeti feki wakati wa kuomba kazi, barua nyingi
zimeonekana kuambatanishwa na nakala feki," alisema.
Aliongeza:
"Ni jambo la kusikitisha kuona mtu anatumia vyeti ambavyo si vyake kwa
lengo la kujipatia kazi kiudanganyifu au wengine wanajaribu kuongeza
vigezo ambavyo hana kwa kazi anayoomba ambapo husababishwa kutoitwa
kwenye usaili,", alisema.
Abraham
alisema kuwa ofisi ya Sekretarieti ya Ajira katika utumishi wa umma
inajipanga kutoa elimu kwa wahitimu na wadau mbalimbali wa elimu katika
kuzitatua changamoto hizo.
Aliongeza
kuwa sekretarieti hiyo katika kukabiliana na changamoto hizo
wanatarajia kuhama katika mfumo wa analojia na kwenda dijitali ambapo
wahitimu na walio Makazini watatuma maombi kwa njia ya kielektroniki
No comments:
Post a Comment