WANANCHI WA KIJIJI CHA CHALANGWA WILAYANI CHUNYA
WAFUNGA BARABARA YA MBEYA/CHUNYA BAADA YA KUWEPO MGOGORO KATI YAO NA
MMILIKI MMOJA WA ENEO LA UCHIMBAJI MADINI.
WANANCHI
WA KIJIJI CHA CHALANGWA WILAYANI CHUNYA MKOA WA MBEYA WAFANYA VURUGU
ZINAZOTOKANA NA WANANCHI KUPINGA KUKAMATWA BAADHI YA WENZAO KUFUATIA
VITISHO NA VURUGU WANAZOMFANYIA MMOJA WA WAMILIKI WA ENEO LA UCHIMBAJI
WA MADINI LENYE LESENI NA. 0003904 KWA MADAI KUWA SI MKAZI WA KIJIJI
HICHO NA HIVYO KUTAKA KUMNYANG`ANYA ENEO LAKE. VURUGU HIZO ZILITOKEA
MNAMO TAREHE 02/03/2014 MAJIRA YA ASUBUHI AMBAPO WANANCHI WA KIJIJI CHA
CHALANGWA WALIZIBA BARABARA YA MBEYA/CHUNYA KWA KUTUMIA MAGOGO NA MAWE
WAKISHINIKIZA POLISI KUTOWAKAMATWA WANANCHI WENZAO
AWALI
WANANCHI HAO MNAMO TAREHE 19/02/2014 SAA 10:00HRS KATIKA KITUO CHA
POLISI CHUNYA YALIPOKELEWA MALALAMIKO TOKA KWA JOSEPH LAISON @ MWAZYELE
(47), MKAZI WA KIJIJI CHA KIWANJA KATA YA MBUGANI, TARAFA YA KIWANJA
KUWA MNAMO TAREHE 18/02/2014 MAJIRA YA SAA 09:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI
CHA CHALANGWA ALITISHIWA KUUAWA NA WANANCHI WATANO (5) ALIOWATAJA KUWA
NI 1. JOSEPH RASHID, 2. MWAMBO MWAGANE 3. TEDY MWAGANE 4. MEDY KATEMBO
NA 5. VENACERASHID NA HIVYO JALADA LA KUTISHIA KUUA KWA MANENO
LILIFUNGULIWA. MLALAMIKAJI HUYO KATIKA MAELEZO YAKE ANASEMA KUWA CHANZO
CHA TUKIO HILO NI KIWANJA CHA KUCHIMBA MADINI AINA YA DHAHABU
ANACHOKIMILIKI KILICHOPO KATIKA KIJIJI CHA CHALANGWA CHENYE LESENI
(PRIMARY MINING LICENCE) NAMBA 0003904 TANGU TAREHE 03/05/2004 AWALI
KILIKUWA NA UKOMO WA KWANZA TAREHE 02/05/2006 HATA HIVYO ALIENDELEA
KUKILIPIA NA SERIKALI ILIONGEZA MUDA WA LESENI TAREHE 16/03/2004 HADI
02/05/2011 NA BAADAE KUKILIPIA NA KWA MARA YA MWISHO ALIONGEZEWA KIBALI
CHA UMILIKI TAREHE 19/10/2012 HADI 02/05/2018.
HATA
HIVYO KABLA YA HATUA ZOZOTE ZA KUPAMBANA NA WANANCHI HAO HAZIJAANZA
KUCHUKULIWA MKUU WA WILAYA YA CHUNYA NDG DEODATUS KINAWIRO ALIFIKA
KIJIJINI HAPO NA KUONGEA NA WANANCHI KWA NJIA YA KIDIPLOMASIA MAZUNGUMZO
YALIYOFUATIWA NA UTOAJI WA MAELEKEZO NA MSIMAMO WA SERIKALI YA WILAYA
KWA WANANCHI HAO. KATIKA MAZUNGUMZO HAYO MAMBO MATATU YALIELEKEZWA
KUTEKELEZWA AMBAYO NI 1.MARUFUKU WANANCHI WA KIJIJI HICHO AU MCHIMBAJI
HUYO KWENDA KUCHIMBA DHAHABU ENEO HILO LENYE MGOGORO MPAKA HAPO MGOGORO
HUO UTAKAPOTATULIWA NA SERIKALI 2. MARUFUKU WANANCHI KUJICHUKUA SHERIA
MKONONI HASA KUFUNGA BARABARA NA KULETA VURUGU KWANI HILI INAONYESHA NI
TUKIO LA TATU (3) KIJIJINI HAPO 3. WILAYA YA CHUNYA NI YA WACHIMBAJI
MADINI NA KWAMBA LESENI ZAO ZINATOLEWA NA KAMISHNA WA
MADINI DAR ES SALAAM NA LAZIMA LESENI HIZO ZIHESHIMIWE NA WANANCHI
WAACHE KUVAMIA MAENEO YENYE LESENI NA KWAMBA SERIKALI HAITAVUMILIA
VITENDO HIVYO VINAVYOTAKA KUOTA MIZIZI. KATIKA MAZUNGUMZO HAYO AMBAYO
WANANCHI WALIONEKANA KUMWELEWA MKUU WA WILAYA HIYO, WALIMWOMBEA
MTUHUMIWA ALIYEKUWA AMEKAMATWA NA POLISI AACHILIWE HURU BAADA YA KUWA
AMEJISALIMISHA MWENYEWE KATIKA MKUTANO HUO.
AMANI
KATIKA ENEO HILO IMEREJEA MAJIRA YA SAA 11.00 HRS NA BARABARA YA
MBEYA/CHUNYA KUFUNGULIWA. HAKUNA MADHARA YOYOTE YA KIBINADAMU
YALIYORIPOTIWA KUJITOKEZA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUTUMIA NJIA ZA MAZUNGUMZO KUTATUA MIGOGORO/KERO ZINAZOWAKABILI KATIKA
MAENEO YAO NA KUACHANA NA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MIKONONI KWANI
NI KINYUME CHA SHERIA.
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI MKOANI MBEYA.
MTEMBEA
KWA MIGUU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA MOJA LA MWAKYEMBE, MWENYE UMRI
KATI YA MIAKA 30-35, ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI
LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 430 APD AINA YA TOYOTA COROLLA LILILOKUWA
LIKIENDESHWA NA GREYSON PONELA (30) MKAZI WA ILEMI. TUKIO HILO LILITOKEA
MNAMO TAREHE 02.03.2014 MAJIRA YA SAA 22:49HRS USIKU HUKO MWANJELWA
KATA YA MANGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI
KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
DEREVA AMEKAMATWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA
MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA
USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA
WITO KWA WATEMBEA KWA MIGUU KUWA MAKINI KWA KUTEMBEA PEMBEZONI MWA
BARABARA NA KUVUKA SEHEMU AMBAZO KUNA VIVUKO VYA KUVUKIA [ZEBRA
CROSSING].
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATATU WAKIWA NA MALI IDHANIWAYO KUWA YA WIZI.
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATATU 1. EMMANUEL JAILOS
(30) MKAZI WA MADABAGA 2. ANNA NURU (26) NA 3. MOHAMED HEMED (20) WOTE
WAKAZI WA IGURUSI WAKIWA NA MAFUTA YA DIESEL LITA 600, MAPIPA 04 YA
DIESEL, MADUMU 13 YA DIESEL, MADUMU MATUPU 40 NA MBOLEA YA ZAMBIA MIFUKO
05 MALI IDHANIWAYO KUWA NI YA WIZI. WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA KATIKA
MSAKO MAALUM ULIOENDESHWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA MNAMO TAREHE
02.03.2014 MAJIRA YA SAA 00.01HRS USIKU HUKO KIJIJI NA KATA YA MADABAGA,
TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA WATUHUMIWA
MAHAKAMANI ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI
KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOWATILIA MASHAKA KATIKA MAENEO YAO JUU YA
KAZI/SHUGHULI WANAZOFANYA IKIWA NI PAMOJA NA MAKUNDI YA VIJANA
WANAOJIHUSISHA NA WIZI WA MAFUTA KATIKA MAGARI YANAYOSAFIRISHA BIDHAA
HIYO ILI WAKAMATWE NA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
WATU WATATU WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA NOTI BANDIA.
WATU
WATATU WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. ALEX FUNGAI (25) 2. TIMOTHY MGINA
(27) NA 3. LUSEKELO STEPHANO (20) WOTE WAKAZI WA MBEYA MJINI
WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA NOTI BANDIA 13
ZA TSHS 10,000/= ZENYE THAMANI YA TSHS 130,000/= ZIKIWA NA NAMBA BX
8365292 NOTI SABA, NAMBA BX.8365294 NOTI MBILI, NAMBA BL. 6882315 NOTI
MBILI NA BX.5764841 NOTI MBILI. WATUHUMIWA KWA PAMOJA WALIKAMATWA MNAMO
TAREHE 02.03.2014 MAJIRA YA SAA 18:13HRS JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA
IBALA, KATA YA RUJEWA, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI MKOA WA
MBEYA. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA WANANCHI NA WAFANYABIASHARA KWA UJUMLA KUWA MAKINI NA
WATU WANAOKUJA KATIKA MADUKA YAO HASA KATIKA SEHEMU ZA KUTUMA NA KUWEKA
FEDHA KWA NJIA YA SIMU ZA MKONONI ILI KUEPUKA UDANGANYIFU UNAWEZA
KUFANYWA NA WATU HAO. AIDHA ANATOA WITO KWA RAIA WEMA KUENDELEA KUTOA
TAARIFA KWA JESHI LA POLISI JUU YA MTU AU KUNDI LA WATU WANAOJIHUSISHA
NA UTENGENEZAJI/USAMBAZAJI WA NOTI BANDIA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZAIDI
ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Signed by
[B.N.MASAKI – ACP]
Kny: KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
No comments:
Post a Comment