KATIBU TAWALA WA MKOA BW. BENEDICTOR OLE KUYAN AKIZUNGUMZA NA WAADISHI WA HABARI MCHAN WA LEO.
MWANDISHI
WA HABARI WA CHANNEL TEN AUGASTINE MGENDI AKIMUULIZA KATIBU TAWALA
SWALI HUKU WAANDISHI WENGINE WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI.WAKATI WAKIPOKEA
RATIBA YA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU TOKA KWA KATIBU TAWALA.
--
NA AHMAD NANDONDE,
MUSOMA.
MWILI
WA ALIYEKUWA MKUU WA MKOA WARA BW. JOHN TUPPA UNATARAJIA KUAGWA KESHO
NYUMBANI KWAKE KUANZIA SAA MOJA KAMILI ASUBUH MPAKA SAA TATU NA DK 20
MUSOMA MKOANI MARA NA BAADAE KUELEKA KANISA KUU LA ROMAN CATHOLIC
PAROKIA YA MUSOMA KWAAJILI YA IBADA YA KUMUOMBEA MAREHEMU KUANZIA SAA
TANO ASUBUHI HADI SA 9:00 JIONI.
HAYO
YAMESEMWA LEO NA KATIBU TAWALA WA MKOA BW. BENEDICTOR OLE KUYAN
ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI MCHAN WA LEO KATIKA UKUMBI
MDOGO WA MIKUTANO.
OLE
KUYAN AMESEMA KUWA MARA BAADA YA IBADA HIYO MWILI WA MAREHEMU
UTASAFIRISHWA MPAKA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA MWANZA AMBAPO UTAWASILI
SAA KUMI NA NUSU ALASIRI KABLA YA KUSAFIRISHWA TENA HADI MJINI DODOMA
AMBAPO UNATARAJI KUWASILI SAA KUMI NA MOJA JIONI NA KUHIFADHIWA KATIKA
HOSPITAL YA MKOA.
KWA
KUWA ENZI ZA UHAI WAKE MAREHEMU ALIWAHI KUFANYA KAZI MJINI DODOMA KAMA
MKUU WA WILAYA WANANCHI MKOANI HUMO WATAPATA FURSA YA KUUAGA MWILI WA
MAREHEMU TAREHE 28 KUANZIA SAA TATU ASUBUHI HADI SAA SITA MCHANA.
BW.
OLE KUYAN AMEONGEZA KUWA BAADA YA WAKAZI WA DODOMA KUUAGA MWILI WA
MAREHEMU SAA SITA MCHANA MWILI HUO UTASAFIRISHWA TENA HADI KIJIJINI
KWAKE KILOSA AMBAPO UTAKABIDHIWA KWA FAMILIA YA MAREHEMU KWAAJILI YA
MAOMBOLEZO SAA TISA ALASIRI.
MWILI
WA MAREHEMU UTAFANYIWA IBADA IKIWA NI PAMOJA NA WANANCHI WA KILOSA
KUUAGA MWILI WA MAREHEMU KWA MARA MWISHO KABLA YA KUPELEKWA KATIKA ENEO
LA MAZISHI KWAA JILI YA KUUHIFADHI KATIKA NYUMBA YA MILELE SAA KUIMI NA
MOJA JIONI.
MAREHEMU TUPA AMEFARIKI DUNIA JANA WILAYANI TARIME ALIPOKUWA KATIKA ZIARA YAKE YA KIKAZI NA AMEACHA MKE NA WATOTO WATANO.
MAREHEMU ALIZALIWA JAN 1 1950.
MWISHOOOO…
----
TAARIFA TOKA TAASISI YA WAANDISHI WA HABARI MKOANI MARA YA MARA HOPE FOR LIFE (MHL) BIGAMBO JEJE,MUSOMA MARCH 26 2014,
TUPPA.
TAASISI
YA WAANDISHI WA HABARI MKOANI MARA YA MARA HOPE FOR LIFE (MHL)
IMEMTUMIA SALAMU ZA RAMBIRAMBI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MHE:DK JAKAYA KIKWETE KUFUATIA KIFO CHA MKUU WA MKOA WA MARA JOHN
GABRIEL TUPPA ALIYEFARIKI DUNIA KWA GHAFLA AKIWA KATIKA KAZI ZA
KUWATUMIKIA WANANCHI.
MKURUGENZI
MKUU WA TAASISI HIYO YA WANAHABARI WA MKOA WA MARA BW. FAZEL JANJA
AMEMUELEZEA MAREHEMU TUPPA KWAMBA WATANZANIA DAIMA WATAMKUMBUKA KWA
MAMBO MENGI KATIKA KUWATUMIKIA WATANZANIA KATIKA NYADHIFA MBALIMBALI
ALIZOZITUMIKIA KATIKA UADILIFU NA UAMINIFU MKUBWA.
BW.
JANJA AMESEMA WAKATI WA UHAI WAKE HUSUSANI TANGU ALIPOTEULIWA NA RAIS
KIKWETE KUTUMIKIA WADHIFA WA UKUU WA MKOA WA MARA MWAKA 2011, MAREHEMU
ALIJITOLEA KWA HALI YAKE YOTE KUHAKIKISHA ANAWAHUDUMIA WANANCHI KATIKA
KUWALETEA MAENDELEO KATIKA NYANJA KADHAA ZA ELIMU,MIUNDO MBINU,AFYA,MAJI
NA KILIMO HUKU AKIMSIKILIZA KILA MWANANCHI NA KUTATUA KERO ZAO KWA
KUTENDA HAKI BILA AINA YOYOTE ILE YA AMA UBAGUZI AU UPENDELEO.
AMETANABAISHA
KWAMBA MAREHEMU TUPPA AMBAYE KIFO CHAKE NI PIGO KUBWA NA KIMEACHA PENGO
LISILOWEZA KUZIBIKA KWA URAHISI, ENZI YA UHAI WAKE ALISHIRIKIANA NA
VYAMA VYOTE VYA SIASA KATIKA SHUGHULI ZA KIMAENDELEO HUKU AKIWAITA NA
KUKAA NAO ILI KUJADILI NAMNA YA KUWEZA KUUENDELEZA MKOA KWA KUSHIRIKIANA
KWA PAMOJA BILA KUWEKA TOFAUTI ZA VYAMA VYAO.
SALAMU
HIZO ZA RAMBIRAMBI KWENDA KWA MHE:RAIS KIKWETE ZIMEONGEZA KUWA
WAANDISHI WA HABARI MKOANI MARA WALIPATA USHIRIKIANO MKUWA NA WA KARIBU
SANA TOKA KWA MAREHEMU TUPPA AMBAYE DAIMA ALIWAPENDA WANAHABARI NA
KUWAPA KILA AINA YA USHIRIKIANO WALIOUTAKA TOKA OFISINI KWAKE NA KWAMBA
KIFO CHAKE KIMEACHA PIA MAJONZI,SIMANZI NA HUZUNI ISIYO NA KIFANI KWA
WANAHABARI WOTE.
MKURUGENZI
HUYO MKUU WA TAASISI HIYO YA MHL BW. JANJA AMEWATAKA VIONGOZI KUIGA
MFANO WA MAREHEMU TUPPA KATIKA KUWATUMIKIA WANANCHI KWA KILA HALI NA KWA
MOYO WA KUJITOLEA NA KUSISITIZA KUWA HATUA YA KUKUTWA NA UMAUTI AKIWA
KAZINI NI USHUJAA,USHUPAVU NA UJASIRI MKUBWA AMBAO DAIMA JINA LAKE
LITAANDIKWA KATIKA HISTORIA YA MASHUJAA WA HAPA NCHINI.
AIDHA
AMEIOMBA FAMILIA YA MAREHEMU ALIYEFARIKI KUTOKANA NA SHINIKIZO LA DAMU
AKIWA KIKAZI WILAYANI TARIME, KUWA NA UVUMILIVU,USTAHIMILIVU NA SUBIRA
KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU WANACHOPITIA NA KUJIPA MOYO INGAWA KILA MMOJA
ANATAMBUA KWAMBA MAREHEMU AMETANGULIA MBELE ZA HAKI HUKU FAMILIA HIYO
IKIWA BADO INAMUHITAJI.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment