Kaka wa Satrin Osinya, Moses Gift akiwa amembeba mdogo wake baada ya kunusurika kifo.
MTOTO
Satrin Osinya aliyejeruhiwa na risasi iliyomuua mama yake katika
shambulio la kigaidi lililofanywa kwenye kanisa la Joy of Jesus huko
Likoni, Mombasa nchini Kenya Jumapili iliyopita, jana amefikishwa jijini
Nairobi kwa matibabu.
Mtoto Satrin Osinya wakati akipatiwa matibabu mjini Mombasa baada ya kupigwa risasi.
Osinya
mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa
kichwa katika Hospitali Kuu ya Kitaifa ya Kenyatta ili kuondoa risasi
iliyoingia kwenye ubongo wake baada ya kumuua mama yake.
Madaktari
wanasema kuwa ubongo wa mtoto huyo umefura na kwamba risasi iko upande
wa kulia wa ubongo wenyewe. Upasuaji unatarajiwa kufanywa baada ya wiki
mbili ambao utagharamiwa na serikali.
Mtoto Satrin akiwa amebebwa na baba yake mzazi Benson Osinya ndani ya ndege kuelekea jijini Nairobi kwa matibabu.
Mama
mzazi wa Satrin aliyekuwa akijaribu kumkinga mwanaye kutoka kwa magaidi
waliovamia kanisa la Joy of Jesus siku ya Jumapili, alifariki kanisani
humo baada ya kupigwa risasi. Inadaiwa risasi aliyomuingia kichwani
Satrin ni risasi iliyomuua mama yake kupitia kifuani na kuishia katika
ubongo wa mtoto huyo.
Mamake
Satrin, alikuwa miongoni mwa watu sita waliouawa katika shambulizi
hilo, baada ya washukiwa watatu wa ugaidi kulivamia kanisa hilo katika
mtaa wa Likoni na kuanza kuwafyatulia waumini risasi kiholela.
No comments:
Post a Comment