Familia za abiria wa ndege iliyotoweka ya Malaysia wakiandamana wakiwa wamebeba mabango.
Mkusanyiko wana familia za abilia wa ndege iliyotoweka ya Malaysia wakiendelea na maandamano.
Polisi wakiwatuliza wana familia wenye hasira kali.
Familia
za abiria wa ndege iliyotoweka ya Malaysia majuma mawili yaliyopita,
wamekabiliana na polisi nje ya ubalozi wa Malaysia mjini Beijing.
Wakiwa wamejawa na ghadhabu, wamelitaka shirika la ndege ya taifa hilo mjini Kuala Lumpur kueleza kilIchofanyika.
Jamaa
hao walibeba mabango yenye maandishi "Save MH370" jamaa hao wenye hasira
walikabiliana na polisi na kuwalemea hadi kuingia katika ofisi ya
ubalozi huo.
Walifoka wakisema ..''Tunataka ukweli." hii ni ishara ya hasira na mafadhaiko wanayopitIa jamaa hao wa watu waliopotea.
Kero la
jamaa hao limekuja baada ya waziri mkuu wa Malaysia, Najib Razak kusema
udadisi wa data ya Satelite ulionyesha kuwa safari ya ndege hiyo
iliishia baharini Kusini mwa Australia.
Serikali ya China imeomba kuona data hiyo ambayo Malaysia imeamini kiasi cha kutoa msimamo wake.
Msako wa ndege hiyo umesitishwa kutokana na mawimbi makali baharini
Shughulii ya kuitafuta ndege hiyo MH370 imesitishwa kutokana na mawimbi makali baharini.
Mataifa
mbali mbali yalijitolea kusaidia Malaysia kuitafuta nmdege hiyo, juhudi
ambazo zililengwa zaidi katika bahari ya Kusini Magharibi mwa mji wa
Australia Perth
Ndege
hiyo MH370 ilipotea tarehe nane mwezi Machi, ilipokuwa njiani kuelekea
Beijing kutoka Kuala Lumpur.Ilikuwa imebeba abiria 239 ikiwemo raia 153
wa China.
Maandamano
ya umma ni haramu nchini China,lakini hadi kufikia watu hawa wakapanga
maandamano kama hayo ni ishara kuwa hawana kilichobakia kuwapa matumaini
kabisa
No comments:
Post a Comment