THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TANGAZO
LA SERIKALI KUHUSU KUVUNJWA KWA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA
Mhe.
Rais aliunda Tume ya Mabadiliko ya Katika kwa mujibu wa kifungu cha 5 na 6 cha
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 kwa Tangazo la Serikali Na.110 la
Mwaka 2012.
Tume
ilikusanya maoni na kuandaa Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ambayo imewasilishwa kwenye Bunge Maalum.
Kwa
mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 3, Rais
amepewa mamlaka ya kuvunja Tume ya Mabadiliko ya Katiba baada ya Rasimu ya
Katiba kuwasilishwa Bungeni.
Mnamo
tarehe 18 Machi, 2014 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph
Sinde Warioba aliwasilisha Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalum. Kutokana na hatua hiyo, na kwa mujibu wa
kifungu cha 31 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Rais wa Jamhuri ya Muungano
alivunja rasmi Tume ya Mabadiliko ya Katiba tarehe 19 Machi,2014 kwa Tangazo la
Serikali Na.81 la tarehe 21 Machi, 2014.
Hivyo
kwa Tangazo hilo, shughuli zote za Tume ya Mabadiliko ya Katiba zimemalizika
rasmi tarehe 19 Machi, 2014.
Imetolewa
na;
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
Dar es Salaam.
25
Machi,2014
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399
No comments:
Post a Comment