Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, March 4, 2014

UNAMKUMBUKA YULE BONDIA FRANK BRUNO...SASA NI MTENGENEZA NYWELE WANAWAKE SALUNI JIONEE HAPA


MBABE wa zamani ulingoni, Frank Bruno amesema amerudi mazoezini tena, lakini safari hii akijifua kuwa mtengeneza nywele za wanawake saluni.

Bingwa huyo wa zamani wa dunia wa nsonsi za kulipwa mwenye umri wa miaka 52 sasa alikumbana na suluba nyingi enzi zake ulingoni.

Lakini baada ya msoto wa kutafuta msimamo mpya wa maisha tangu astaafu mwaka 1996, inatokea anataka kuhamishia umahiri wake wa ulingoni kwenye nywele za mabinti.



Wapendanao: Frank Bruno akiwa na mpenzi wake,Nina Coletta ambaye anamsaidia kujifunza kazi za kutengeneza nywele za wanawake



Legends: Bruno in action against heavyweight champion Mike Tyson at the Hilton in Las Vegas in 1989
Gwiji: Bruno akizipiga na bingwa mwingine wa zamani wa uzito wa juu, Mike Tyson ukumbi wa Hilton mjini Las Vegas mwaka 1989
Sura ya maumivu: Bruno katika picha hii aliyopigwa Januari 2014 kwenye shughuli ya hisani, sasa anaweza kuwa mtengeneza nywele wanawake saluni

A cut above: Bruno, pictured in January 2014 at a charity event, could move into a new line of work as a hairdresser


Bruno ametweet Ijumaa: "Ninajifunza hairdressing (utengenezaji nywele) wazo lolote la jina la saluni? Itakuwa tayari miaka michache (ijayo),".

Mkazi huyo wa London amekuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mtengeneza nywele Nina Coletta ambaye ana saluni yake mjini Glasgow, na wawili hao wamekuwa karibu mno na sasa anataka kufanya kazi pamoja naye.

Mwaka 2012 Bruno alikuwa akitibawa katika kliniki ya Glasgow na ndipo alipokutana na Coletta katika harusi ya rafiki yake kwenye jiji hilo la Scotland.

Katika mahojiano aliyofanyiwa mwaka huo, Bruno alinukuliwa akisema: "Amenisaidia kuliko uwezo wake. Namhitaji kuliko anavyonihitaji. Mwaka huu amenisaidia kutoka kwenye maradhi na kurudi katika uimara wangu,".

Bruno amebaki kuwa mtu maarufu tangu astaafu ndondi na bado anapambana na kumudu hali ya maisha nje ya ulingoni na aligundulika kuwa na maradhi ya uchizi katika hospitali ya Mental Health Act mwaka 2003.


Sporting great: Former boxer Bruno takes a turn carrying the Olympic flame around London in 2004
Bondia wa zamani, Bruno akiwa ameshika mwenge wa Olimpiki mjini London mwaka 2004



Heyday: Bruno, in the ring with Joe Bugner at White Hart Lane, won 40 of his 45 bouts, with 38 by knockout
Bruno, ulingoni akizipiga na Joe Bugner Uwanja wa White Hart Lane, enzi zake alishinda mapambano 40 kati ya 45 aliyopigana, 38 kati ya hayo kwa Knockout (KO).

No comments:

Post a Comment