Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, March 14, 2014

UTAFITI: UTUMIAJI ULIOZIDI WA SIMU KWA WAZAZI HUPUNGUZA UKARIBU NA WATOTO WAO

Watafiti kutoka Boston Medical Centre wamebaini kuwa matumizi yaliozidi ya simu kwa wazazi hupunguza mapenzi kutoka kwa watoto wao.
Katika utafiti waliofanya, waligundua kuwa mmoja kati ya wazazi watatu hutumia simu mara kwa mara wakati wa chakula na huku utafiti mwingine ukidai kuwa kukosekana kwa kutazamana machoni na mazungumzo ya kawaida hupunguza ukaribu na watoto wao.
Katika utafiti huo waligundua tabia tano za wazazi kuanzia wazazi wasiotumia kabisa simu zao wakati wa chakula, wazazi wanaoweka simu zao mezani bila kuzitumia, wazazi wanaotumia simu mara chache wakati wa kula, wazazi wanaotumia simu baada ya chakula na wale wanaotumia simu muda wote.
Watafiti hao wamebaini kuwa pale wazazi wanapotumia muda mwingi kuangalia simu zao, watoto wao huanza kufanya fujo kutaka attention.
“Wazazi wanaojikuta wakitumia sana simu zao wanaonekana kuwa na maongezi hafifu na watoto wao,” alisema Dr Jenny Radesky

No comments:

Post a Comment