Cosmas Njingo-afisa habari na mawasiliano wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro akichangia mada.
Zadock Kitomary-Mkulima bora mara mbili mfululizo katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mkoani Arusha akitoa mada.
Ayubu Nnko-Msimamizi wa Jarida kwa upande wa Tanzania akitoa mada katika Semina hiyo.
Coroline Nyakundi- Meneja Mradi The Organic Farmer& jarida la Mkulima mbunifu akitoa mada.
John Cheburet-Mtayarishaji wa vipindi vya Redio kutoka jarida la Mkulima mbunifu .

Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali na Mafunzo katika semina hiyo
******
Na Arusha yetu Blog
IMEELEZWA kuwa Watanzania ni
wavivu wa kusoma Majarida mbali mbali yanayoweza kuwaongezea upeo ukilinganisha
na nchi zingine.
Hayo yamebainishwa na Mmoja wa
maafisa wa Jarida la Mkulima Mbunifu, Caroline Nyakundi kutoka Nchini Kenya,
wakati akizungumza katika mafunzo ya waandishi wa habari za kilimo na wataalamu
wa kilimo yanayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Arusha Crown ya Mjini hapa.
Ameongeza kuwa kunatofauti
kubwa ya Mwitikio wa kusoma machapisho kati ya Raia wa Tanzania ukilinganisha
na Kenya ambako imeelezwa kuwa wanauhitaji mkubwa wa kujifunza mbinu mpya za
kilimo tofauti na Watanzania ambao hawana uhitaji wa kusoma na kutaka kujua
zaidi.
Akieleza Mikakati ya Jarida la
Mkulima Mbunifu mmoja katika ya Maafisa wa Jarida hilo, Caroline Nyakundi kutoka
Nchini Kenya, amesema tangu kuzinduliwa kwa jarida hilo Juni,2011 limeonesha
mwitikio mkubwa kutokana na kupata taarifa nyingi kutoka kwa wakulima
wakilihitaji ili kujua zaidi habari za Kilimo.
Amesema Jarida hilo limelenga
zaidi maoni na mahitaji ya Mkulima kutokana na mawazo yao ambayo wamekuwa
wakiyatoa katika jarida hilo mara kwa mara jambo linaloonesha Mkulima kufikiwa
na Jarida hilo na kwa wakati.
No comments:
Post a Comment