Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, April 13, 2014

DARAJA LA LINALOUNGANISHA BAGAMOYO NA DAR LAANZA KUJENGWA BAADA YA KUSOMBWA NA MAFURIKO



Wakazi wa eneo la Mapinga Mkoani Pwani wakiwa kwenye mshangao mkubwa baada ya kushindwa kuvuka Daraja la Mto unaokatisha kwenye eneo hilo baada ya kutokuwepo kwa mawasiliano ya barabara kwa kukatika kwa daraja hilo kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hivi sasa katika maeneo mbali mbali hapa nchini.

Akithibitisha kutokea kwa hitilafu hiyo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, ACP Ulrich Matei amesema ni kweli kumetokea kwa tatizo hilo na amewataka watumiaji wa barabara ya Bagamoyo kubadilisha njia na kuwanza kutumia barabara ya Morogoro mpaka hapo daraja hilo litakapofanyiwa matengenezo.


Wakati jitihada zikifanyika kurudisha mawasiliano ya barabara na 
makamanda wakitafakari juu ya kuweka daraja la muda, watu wameanza 
lawama eti mkandarasi. Lakini ukweli ni mambo ni matatizo yetu wenyewe. 
Ukiangalia kati ya hizi picha, kuna moja inaonekana na matete katikati 
na pembeni yake, kushoto na kulia yanapita maji. Maeneo haya yanayopita 
maji kwa kipindi fulani yalikuwa yakichimbwa mchanga na kuacha katikati 
ya mto kuwa na mwinuko. Mvua nyingi maji yamepita pembeni na hata kwenda
nje ya daraja.




 Mawasiliano kati ya Dar na Bagamoyo kwa barabara ya Bagamoyo yamekatika.
Maji yanayopita katika mto Mpigi ambako daraja halipitiki ni mengi sana
kiasi kwamba nguzo tatu zinazopitisha umeme mkubwa kwenda Bagamoyo zipo
hatarini. Mojawapo maji yanaikaribia zaidi na uwezekano wa kusombwa ni 
mkubwa kwa sababu miti mikubwa iliyokuwa karibu na eneo hilo nayo 
imeng'olewa kirahisi kabisa. 

No comments:

Post a Comment