Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, April 26, 2014

MBARONI KWA KUKUTWA NA MIKIA YA TEMBO RUVUMA

Na Gideon Mwakanosya- Songea
Jeshi la polisi Mkoani Ruvuma limemtia mbaroni Idd Kiambwe Ndomondo (30) mkazi wa kijiji cha Silabu Wilayani Masasi Mkoa wa Mtwara kwa tuhuma za kukutwa na mikia ishirini ya tembo yenye thamani ya dola za Kimarekani 300,000 ambazo ni sawa na shilingi za Kitanzania 480,000,000.



Habari zilizopatikana jana mjini Songea ambazo zimethibitishwa na Kamanda wa Poliosi wa Mkoa wa Ruvuma Akili Mpwapwa zimesema kuwa tukio hilo lilitokea Aprili 21 mwaka huu katika eneo la Biasi lililopo kata ya Nakayaya wilayani Tunduru.


Mpwapwa alifafanua zaidi kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio majira ya asubuhi askari polisi waliokuwa kwenye kazi maalumu walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa Ndomondo akiwa ameficha nyara hizo kwenye begi jeusi akisafiri nazo kuelekea Masasi mkoani Mtwara.


Alisema kuwa mtuhumiwa Ndomondo baada ya kuhojiwa na kugundua kuwa lile begi ni la kwake walimkamata na kumrudisha Kituo Kikuu cha Polisi cha Tunduru ambako anashikiliwa na kwamba polisi wanaendelea kumhoji zaidi.


Kamanda Mpwapwa alieleza zaidi kuwa mtuhumiwa Ndomondo anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili mara tu upelelezi utakapokamilika.

No comments:

Post a Comment