Mamba aliekua akiishi katika ziwa
Victoria mwenye umri wa miaka 80, mwenye uzito unaokadiriwa kukaribia
tani moja amekamatwa katika ziwa Victoria upande wa Uganda ni baada ya
wananchi kulalamika kuhusu mamba huyo anaekula watu, huku akikadiriwa
kuwa ameshakula watu wasiopungua sita mpaka kukamatwa kwake

watu wengi kutoka kijiji cha kakira walifika kushuhudia mamba huyo akitolewa majini, huku wakiwa na nyuso za furaha na wengi wakipiga picha


No comments:
Post a Comment