Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, May 10, 2014

AJALI YAUA MWANAFUNZI WA MIAKA 11 MBEYA

Mwanafunzi wa shule ya msingi Jangurutu darasa la tano aliyetambulika kwa jina la Habibu Dismass (11) amefariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na gari lenye namba za usajili T.120 AMV aina ya Camry lililokuwa likiendeshwa na derava Otino Mwampamba (48) mwalimu shule ya sekondari, Mbarali.

Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 10:15 jioni huko katika kijiji cha Mabanda, kata na tarafa ya Rujewa wilaya ya Mbarali mkoa wa Mbeya. Chanzo cha ajali ni mwendo kasi. Dereva amekamatwa na gari lipo polisi-Rujewa.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto hasa kwa kuzingatia sheria na alama za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.
Aidha anatoa wito kwa watembea kwa miguu kutembea pembeni mwa barabara na kuvuka sehemu zenye vivuko ili kuepuka ajali.

No comments:

Post a Comment