Mwanamke mmoja nchini Pakistan
amepigwa mawe na familia yake wakiwemo babake na ndugu zake wa kiume hadi
kufariki. Aliuawa nje ya jengo la mahakama mjini Lahore.Mwanamke huyo aliuawa
kwa kuolewa na mtu ambaye alikuwa chaguo lake mwenyewe.
Farzana Bibi, mwenye umri wa miaka
31, aliolewa na Muhammad Iqbal miezi michache iliyopita bila ya idhini ya
familia yake.Polisi wanasema kuwa mwanamke huyo alishambuliwa na familia yake.Kaka
zake na binamu yake mmoja walimshika alipokuwa akiingia mahakamani na kuanza
kumpigwa kwa mawe . Alifariki papo hapo.
Waliomuua walikimbia kabla ya polisi
kufika katika eneo hilo.Babake msichana huyo amekamatwa ingawa washukiwa
wengine wangali hawajulikani waliko.Kwa wanawake wanaoolewa na wapenzi ambao ni
chaguo lao wenyewe, ni kitendo kisichokubalika kitamaduni katika baadhi ya
maeneo ya Pakistan.Mamia ya wasichana huuawa kwa kisingizio cha kuolewa na watu
wasiokubalika na familia zao kila mwakaWanaharakati wa kutetea haki za
binadamu, wanaamini kuwa kwa kuwa mauaji hayo hufanywa na familia zenyewe, huwa
ni vigumu kufikisha kesi hizo kortini.
No comments:
Post a Comment