Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni
Sefue akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Finland nchini Mhe Sinikka Antilla
alipokutana naye Ikulu Dar es salaam Mei 27, 2014.
Balozi Antila ndiye Mwenyekiti wa
Kundi la Nchi 12 Washirika wa Maendeleo zinazosaidia bajeti ya Tanzania
(General Budget Support Group), na amechukua nafasi hiyo tangu mwezi April
mwaka huu.Lengo la Balozi Antila kuonana
na Katibu Mkuu Kiongozi ni kujitambulisha kwa wadhifa huo mpya na kueleza jinsi
atavyotekeleza jukumu hilo la Uenyekiti. Pia ameelezea vipaumbele walivyojiwekea
katika kuchangia bajeti ya serikali na wakabadilishana mawazo ya namna ya
kuimarisha mjadala (dialogue) kati ya kundi hilo la nchi washirika wa maendeleo
na Tanzania.
PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment