Na Mwandishi wetu
Mwanamke mmoja ameuawa
kikatili kwa kukatwa katwa na mapanga sehemu mbalimbali za Mwili wake kwa kudhaniwa
kuwa anaimani za Kishirikina, Mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la Lushiku
Tenganija Sono Msukuma aliyekuwa na Umri
wa Miaka 59 wa kitongoji cha Senga kata ya Bugando Mkoani Geita ameuawa na
mwili kuonekana muda wa Saa moja asubuhi jana ukiwa kwenye
barabara ya mtaa umbali wa mita kama mia tatu kutoka nyumbani alipokuwa akiishi
Marehemu pamoja na wajukuu zake watatu.
Maremu amekatwa shingo
kabisa na kutenganishwa na Mwili, mkono wa kushoto na kulia pamoja na bega la
kulia. Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Bwana Joel Saanane (42) amethibitisha
kutokea kwa Tukio hilo na kudai kuwa msako mkali unaendelea dhidi ya wauaji
hao.
No comments:
Post a Comment