Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, May 2, 2014

Dk Bilal awasili Bukoba kuwasha Mwenge wa Uhuru

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa mjini Bukoba jioni hii kwa ajili ya kuwasha Mwenge wa Uhuru kesho katika hafla itakayofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, Mkoa wa Kagera. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivishwa Skafu na Vijana wa 'Scout' wa mkoa wa Kagera, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa mjini Bukoba jioni hii kwa ajili ya kuwasha Mwenge wa Uhuru kesho katika hafla itakayofanyika kwenye Uwanja wa Kaitaba, Mkoa wa Kagera. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi, waliompokea kwenye uwanja wa Ndege wa mjini Bukoba leo jioni. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment