Na Baby Akwitende, Dar es Salaam
KIKOSI cha wachezaji wakongwe wa timu ya Real Madrid kutoka Hispania kinatarajia kuja nchini kucheza mechi ya kirafiki na nyota wa soka wa Tanzania mchezo utakaofanyika Agosti 23 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa kampuni ya TSN, Dennis Ssebo, alisema kuwa kikosi wawakilishi kutoka Real Madrid ‘Legend Team’.
Timu hiyo ya Real Madrid Legend iliwakilishwa na Mchezaji Mkongwe na kapteni wa timu hiyo Ruben de la Red alieambatana na mchezaji mwingine mkongwe Rayo Garcia pamoja na Isaac Recarey Sanchez anaehusika na maswala ya mahusiano ya Real Madrid Legend Club.
Akizungumza na wana habari mwakilishi huyo wa TSN alisema timu hiyo itawakilishwa na wachezaji 25. Wanatazamiwa kuja kwa siku tatu wakiwa na ratiba mbali mbali. ‘Nje ya mechi ya kirafiki na timu yetu ya Taifa, wachezaji hawa wakongwe ambao bado wako fiti na wanacheza wanatazamia kutembelea mbuga za wanyama kwa minajili ya kuendelea kutangaza utalii wa Tanzania.’ Ratiba ya timu hiyo ni kama ifwatayo:

Naye
mwakilishi na kepteni wa timu ya Real Madrid Legend aliishukuru kampuni
ya TSN kwa kuwapa nafasi ya kuja kuona Tanzania. Wanatambua nchi ya
Tanzania ni moja ya nchi yenye washabiki wa Soka wengi sana na ana amini
mechi yao na vijana wa Tanzania itakua kali na mashabiki
watakaohudhuria watafurahia. Pia aliwashauri vijana wa timu ya Tanzania
kujifua maana yaweza kuwa hawachezi tena kila siku lakini bado wako fiti
na wembe mkali.
Rais
wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) bwana Jamal Malinzi aliipongeza
kampuni ya TSN kwa hatua hii nzuri itakayoongeza tija kwa soka nchini,
machoni mwa ulimwengu wa soka duniani na kuahidi kutoa ushirikiano
kamili kwa TSN kwa ujio huu. “TSN wamefanya jambo la busara sana kwa
soka nchini. Ujio wa timu hii utatupa mafunzo mengi na uzoefu walionao
wachezaji hawa lakini pia watasaidia kuitangaza nchi kwa ujumla. TFF
inaahidi kutoa ushirikiano kamili kwa TSN ili kufanikisha ziara hii”.
TSN imesaini mkataba na wawakilishi wa Real Madrid leo katika hoteli ya Serena. Kwa upande wa TSN Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni hayo Ndugu Farough Baghoza alitia saini kwenye mkataba huo na kapteni wa timu hiyo Ruben De La Red alisaini kwa niaba ya Real Madrid Legends Club.

No comments:
Post a Comment