|
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kushoto akilitazama jeneza lenye mwili wa babake marehemu Frolian Filikunjombe likiingizwa ndani ya kanisa la RC Ludewa kwa ajili ya ibada ya mwisho kabla ya mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Ludewa mjini |
Na Francis Godwin Blog
MBUNGE wa jimbo la Kigoma Kasikazin Zitto (CHADEMleo amegeuka kuwa kivutio kikubwa katika mazishi ya babake mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe huku wananchi wa jimbo hilo na viongozi wa CCM mkoa wa Njombe wakimbebesha majukumu ya ubovu wa barabara kwa kumtaka kushirikiana na mbunge wao kuwasha moto bungeni .
Zitto ambae katika msafara wake huo aliongozana na mbunge wa jimbo la Mwibara Kangi Lugola (CCM) mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga Amina Mwidau (CUF) na wengine wa CCM nusuru avuruge msiba huo baada ya wananchi kuonyesha kuvutiwa na uwepo wake na kumtaka kusikia sauti yake .
Awali wakati wa utambulisho wa viongozi wa kitaifa uliofanywa na mkuu wa wilaya ya Ludewa Juma Madaha waombolezaji baada ya kusikia jina la Zitto Kabwe katika orodha ya wabunge hao ndipo sauti ziliposikika kuwa wanahitaji azungumze .
Hata hivyo katika salam zake katibu wa itikadi na uenezi wa CCM mkoa wa Njombe Honoratus Mgaya mbali ya kumpongeza mbunge Kabwe kwa kufika katika msiba huo na timu yake bado alimtaka Kabwe na timu yake kusaidiana na mbunge wao Filikunjombe kupigania ujenzi wa barabara ya lami kati ya Ludewa na Njombe.
“Mheshimiwa Zitto Kabwe wewe ni mmoja kati ya wapiganaji wa kweli bungeni kama alivyo mbunge wetu na jembe letu wana Ludewa Deo Filikunjombe ….sasa tunaamini mmeona ubovu wa barabara ya Njombe – Ludewa hivyo kupitia ninyi sisi wana Njombe na Ludewa tunaomba msaidiane na Filikunjombe kupigania suala la ubovu wa barabara na sio kutoka nje ya bunge pindi suala la ubovu wa miundo mbinu linapotolewa na mbunge wetu”
Kufuatia ombi hilo la Mgaya waombolezaji walilipuka kwa furaha huku Zitto Kabwe akionyesha kuguswa na ombi hilo na kumtania mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga Amina Mwidau (CUF) kuwa UKAWA hao .
Zitto Kabwe ambae alikuwa ni mmoja wa abiria waliosafiri pamoja na babake Filikunjombe mzee Frolian Filikunjombe kabla ya kufariki dunia akiwa ndani ya ndege kutoka Dubai kuja nchini ni mmoja wa marafiki wakubwa wa mbunge Filikunjombe na pia ni mwenyekiti wa kamati ya PAC ambapo Filikunjombe ni makamu mwenyekiti wake.
Hata hivyo alisema kuwa ombi la wana Ludewa kwake atalifanyia kazi na kuwa suala la siasa lina sehemu yake na yanapozungumzwa mambo ya kimaendeleo siasa za vyama zinawekwa kando .
Hivyo alisema kuwa kutokana na mahusiano mema kati yake ya mbunge Filikunjombe ameguswa na msiba huo na kuwa pindi atakapofika bungeni maombi ya wana Ludewa atayatendea kazi
No comments:
Post a Comment