Mlipuko mkubwa umetokea kwenye meli kubwa ya mafuta nchini
Japan katika Pwani ya Kusini Magharibi mwa bandari ya Himeji na kusababisha mtu
mmoja kati ya wanane waliokuwa ndani ya meli hiyo kupotea huku wengine wanne
wakijeruhiwa vibaya.
Moto mkubwa ulilipuka katikati ya bahari ambapo meli hiyo
yenye uzito wa tani 998 iliyokuwa ikitokea mji wa Hiroshima kuachwa ikielea
ndani ya maji baada ya ajali hiyo na baadae kufatwa na meli za kupambana na
majanga ya moto.
Watu saba wameokolewa katika ajali hiyo mbaya, wanne
wakiuguza majeraha ya moto kwa mujibu wa shirika la habari la NHK, ambapo
kapteni wa meli hiyo amesema uchunguzi kumtafuta mtu mmoja aliyepotea bado
unaendelea.
Afisa usalama katika Pwani hiyo Koji Takarada amesema chanzo cha mlipuko huo bado hakijajulikana ambapo shirika la habari NHK limeripoti kuwa wafanyakazi wa meli hiyo walikuwa wakifanya kazi chini ya meli wakati mlipuko unatoke.
No comments:
Post a Comment