Vijana waliwasha moto magurudumu na kuyaweka barabarani
Kikundi cha vijana wakristo katika Jamuhuri ya Afrika ya
Kati, wameharibu msikiti na kuweka vizuizi barabarani kwa kutumia magurudumu ya
moto mjini Bangui.
Shambulizi hili limekuja siku moja baada ya wapiganaji wa
Seleka, kushambulia kanisa kwa kutumia maguruneti na risasi , huku watu kadhaa
wakiuawa.
Waasi wa Seleka ambao ni waisilamu , wamekuwa wakipigana
vikali na wapiganaji wakristo wanaojiita 'anti-balaka' tangu mwezi Machi mwaka
2013.
Takriban robo ya watu wote nchini CAR, wameachwa bila makao
kutokana na vita.
Hapajakuwa na ripoti zozote kuhusu majeruhi kufuatia
mashambulizi dhidi ya msikiti katika mtaa wa Lakouanga mjini Bangui.
Taarifa kadhaa zilisema kuwa msikiti huo ulikuwa bila watu
wakati wa mashambulizi.
Msemaji wa jamii ya waisilamu wa Bangui, Ousmane Abakar,
aliambia shirika la habari la AP kwamba kwa miezi sita iliyopita,waisilamu
wamekuwa wakishambuliwa huku misikiti ikiharibiwa.
Shambulizi la Jumatano dhidi ya kanisa lilisababisha vifo
vya watu 15 na lilijiri baada ya mapigano katika eneo la PK5 mjini Bangui.Kasisi mmoja wa kanisa hilo, Jonas Bekas, alifahamisha BBC
kuwa wanajeshi wa kulinda amani waliwasili kuchelewa na kukosa kuzuia mauaji.Chanzo BBC
No comments:
Post a Comment