Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, May 16, 2014

WATU WAWILI WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA AJALI YA GARI AINA YA PRADO JIJINI MBEYA


Watu wawili Rehema Mwamaso [30], mkazi wa Sumbawanga na mwanaume mmoja ambaye bado hajafahamika jina wala makazi yake,umri kati ya miaka 30-40, walifariki dunia papo hapo kufuatia ajali iliyotokea wakiwa katika gari T.620 CTL aina ya Toyota Land Cruiser Prado lililokuwa likiendeshwa na dereva Robert Jubery Mwaihoje [61],mkazi wa Sumbawanga.Tukio hilo limetokea  jana majira ya saa 2:00 asubuhi huko katika kijiji na kata ya Nakawale,tarafa ya Ndalambo,wilaya ya Momba, mkoa wa Mbeya, barabara ya Sumbawanga/Tunduma. Katika tukio hilo watu wengine watatu walijeruhiwa akiwemo dereva wa gari hilo na wanawake wawili ambao bado hawajafahamika majina na makazi yao. Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi, taratibu zinafanywa ili dereva afikishwe mahakamani. 


Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa madereva kuwa makini wanapoyumia vyombo vya usafiri kwa kuzingatia sheria na alama za barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika. Aidha anatoa rai kwa wananchi kufika katika kituo cha afya tunduma kwa ajili ya utambuzi wa marehemu na majeruhi.

No comments:

Post a Comment