TAREHE
17.05.2014
SAA 1.00
ASUBUHI CHAI
SAA
4.00-5.00 CHAKULA CHA MCHANA
SAA 5.00-6.00
KUAGA MWILI
SAA 6.00-7.00
MISA KATIKA KANISA KATOLIKI MWANANYAMALA
---------------------------------------------------------------
WASIFU WA PRIVATE BRIAN SALVA RWEYEMAMU
Rwechungura Brian Salva Rweyemamu, aliyefariki
dunia alfajiri ya juzi, Alhamisi, Mei 15, 2014 ni mtoto wa kwanza wa Salva
Rweyemamu na Isabella Kafumba Rweyemamu. Alizaliwa Desemba 27, mwaka 1987,
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar Es Salaam.
Alipata elimu ya awali katika Shule ya Awali ya Mama
wa Kiganda, Kinondoni na Kwa Mama Kate eneo la Chang’ombe, Dar Es Salaam kabla
ya kuhamia Kenya ambako alianza darasa la kwanza katika Shule ya Msingi ya Top
Hill na Lukenya. Hatimaye alihamia kwenye mji Mkuu wa Ubelgiji wa Brussels
ambako aliendelea na elimu ya msingi mwaka 1996.
Brian alijiunga na shule ya Bweni ya Trinity
Exeter nchini Uingereza ambako aliendelea na kumalizia elimu ya msingi. Ili
kumrudisha katika mazingira ya Kitanzania, Bwana Brian alirudia tena darasa la
saba katika Shule ya Msingi ya Julius Nyerere iliyoko Mbezi Beach, Kinondoni,
Dar Es Salaam, mwaka 1998.
Alijiunga na Shule ya Sekondari ya St. Albans ya
mjini Pretoria, Afrika Kusini, mwaka 1999 ambako alikaa miaka minne kabla ya
kujiunga na Shule ya Sekondari ya Kaboja nje kidogo ya mji mkuu wa Uganda wa
Kampala ambako alimaliza kidato cha sita mwaka 2005.
Alijiunga na Chuo Kikuu nchini Malaysia ambako
alichukua masomo ya International Trade, masomo ambayo yalikuwa bado yanamdai
credits za semester ya mwisho kabla ya kuaga dunia.
Alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kambi ya
Mlale, Songea, 2010 na kumaliza kumaliza mafunzo yake mwaka 2011 na hatimaye alijiunga
na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (TPDF) ambako alifanya na kumaliza mafunzo
katika Kambi ya Mafinga mjini Iringa mwaka 06/12/2013 kabla ya kuajiriwa na
JWTZ mwishoni mwa mwaka jana.
Aliomba na kupewa likizo yake ya kwanza ndani ya
JWTZ wiki mbili zilizopita ambako alikaa nyumbani kwa siku chache kabla ya
kushambuliwa na malaria kali wiki iliyopita. Alilazwa Jumamosi iliyopita tarehe
10/05/14 katika Hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugalo akiwa na malaria na kupoteza
fahamu.
Alianza kupata fahamu kwa mbali siku ya Jumanne
usiku na kujaribu kuongea siku ya Jumatano.
No comments:
Post a Comment