Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, May 17, 2014

WAZIRI CHIKAWE AKIWA NA WATENDAJI WAKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI BUNGENI

PIX 1 (4)Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akitoka bungeni baada ya kuwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo katika Bunge la Bajeti linaloendelea mjini Dodoma. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, Mama Anna Abdalla. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PIX 2 (3)Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (watatu kulia), akiwa na maofisa wa wizara hiyo wakati walipokuwa wanatoka bungeni kushuhudia Bajeti ya Wizara yao ilipokuwa ikiwasilishwa katika Bunge la Bajeti linaloendelea mjini Dodoma.  Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PIX 3 (3)Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto-mstari wa katikati), Naibu Katibu Mkuu, Mwamini Malemi (wapili-mstari wa chini) wakiwa na maofisa wa wizara hiyo bungeni wakifuatilia kwa makini wakati Bajeti ya wizara yao ikiwasilishwa bungeni Dodoma. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

PIX 4 (1)
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, Mama Anna Abdalla, nje ya lango Kuu la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Waziri Chikawe tayari amewasilisha Bajeti ya wizara yake katika Bunge la Bajeti linaloendelea mjini Dodoma. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

No comments:

Post a Comment