Mgoni, Nuru Makala ‘Baba Eliza’ (42) aliyefumaniwa akiwa na
mke wa mtu
AMA kweli duniani kuna vituko! Mkazi wa Mtaa wa Lagos, Wazo
Mivumoni, Msitu wa Pande jijini Dar es Salaam, Nuru Makala ‘Baba Eliza’ (42)
Jumatano iliyopita alikumbwa na majanga baada ya mwanaume aliyejulikana kwa
jina la Yusuf Ally ‘Mgosi wa Ndima’ kudai amemfumania Baba Eliza akiwa na mkewe
ambaye jina halikupatikana.
Tafrani hiyo ilijiri usiku wa Jumatano iliyopita, Juni 18,
mwaka huu kwenye nyumba yake iliyopo Mtaa wa Lagos, Msitu wa Pande.
Usiku wa tukio, Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ilikuwa katika
harakati za kusaka matukio katika Jiji la Dar, ndipo ilipokumbana na kelele za
watu waliokuwa wakijibizana.
Ilibidi OFM itie timu kwenye nyumba hiyo na kukutana na
chanzo kimoja kilichodai kuwa baba mwenye nyumba hiyo anadai kumfumania jirani
yake na mkewe kitandani.
Mke wa Bw. Yusuf Ally ‘Mgosi wa Ndima’ akiondolewa eneo la
tukio.
OFM YATINGA NDANI, YAKUTA MAKUBWA
OFM ilizama ndani ya nyumba hiyo na kukuta purukushani kali
ikiendelea, Yusuf akiwa amepandwa na jazba ambapo katika kumkurupusha mgoni
huyo alijigonga mahali na kuumia usoni
“Nilipomuuliza mke wangu alikiri, akasema amekuwa akimwambia
jirani yangu kwamba haiwezekani lakini jamaa anakomaa tu anamwambia wakutane,
tena wakutane humu ndani.
“Ndipo nilipoamua kumuandaa mke wangu kwa mtego amwambie
jamaa kuwa leo (siku ya tukio) sitakuwepo na sitarudi ili kumpa nafasi jamaa
kuja kujinafasi. Baada ya kukamilisha mtego niliwasiliana na kamanda wa
sungusungu wa eneo hilo, Kapteni Makumba na kumuelezea kinagaubaga.”
MTEGO WAANDALIWA
“Kapteni Makumba aliwaandaa vijana wake ambapo kuanzia
mishale ya saa mbili usiku walijibanza kwenye kichaka kilichopo mbele ya nyumba
huku akifanya mawasiliano na mimi.”
JAMAA ATIA TIMU NA KIFURUSHI CHA MACHUNGWA
Yusuf aliendelea kudai kuwa, ilipotimu saa tano usiku kukiwa
kumetulia, Baba Eliza alionekana akikaribia nyumba ya jirani yake huyo kwa
hatua za kunyata na kuangalia kulia na kushoto kisha akazama ndani huku mkononi
akiwa ameshika kifurushi kilichobainika baadaye kwamba kilikuwa na machungwa
kadhaa.
Alisema muda mfupi baada ya kuingia, sungusungu mmoja
alikwenda kujibanza kwenye dirisha la chumba na kupiga chabo kilichokuwa kikiendelea
ambapo alimshuhudia Baba Eliza akichojoa nguo chapchapu tayari kwa mtanange,
sungusungu huyo akawatonya wenzake.
SUNGUSUNGU WACHOMOKA KICHAKANI
Yusuf akazidi kusema kwamba wote walitoka kichakani na
kwenda kuvamia chumbani ambapo walimkuta mkewe aliyekuwa bado hajaanza kuvua
nguo kwa sababu alijua majanga yatatokea muda si mrefu akiwa anajiandaa kufanya
hivyo kiaina.
...Raia aliyeshuhudia mkasa huo akionesha sehemu ya
kitanda iliyochafuliwa na mgoni kwa
kinyesi.
APIGWA FAINI
Wakati OFM ikiwepo eneo hilo, sungusungu walimtaka Baba
Eliza kumlipa fidia Mgosi wa Ndima kwa kitendo cha kumdhalilishia ndoa yake.
Mpaka OFM inaondoka eneo la tukio saa sita na ushee usiku,
Baba Eliza alikuwa katika harakati za kumlipa fidia ya shilingi milioni moja
mwenye mke.
No comments:
Post a Comment