Filipo Inzaghi ateuliwa kocha mpya wa AC Milan
AC Milan imemfuta kazi mkufunzi wake Clarence Seedof baada
ya kuhudumu kwa chini ya miezi 5 na kumtangaza Filipo Inzaghi kama kocha mpya.
Seedof mwenye umri wa miaka 38 alikuwa amechukua nafasi yake
Massimiliano Allegri mwezi Januari, wakati timu hiyo ilikuwa katika nafasi ya
11 katika ligi kuu ya Italia Serie A na alama 30 nyuma ya viongozi wa wakati
huo Juventus, ambao walishinda taji hilo mwisho wa msimu.
Filipo Inzaghi ameteuliwa kocha mpya wa AC Milan na kuchukua
pahala pa Clarence Seedof
Hata hivyo, mholanzi huyo alishindwa kubadili mkondo na
msururu wa matokeo duni uliendelea hadi mwisho wa msimu timu hiyo ilipomaliza
ikiwa na alama 45 nyuma ya mabingwa msimu huu Juventus.
No comments:
Post a Comment