Gari lenye namba za usajili T 894 BEN Toyota Corola lililokuwa likiendeshwa na mwanamama aliyekuwa na watoto wake wawili limepata ajali kwa kutumbukia kwenye mtaro eneo la Mivinjeni, Kurasini Dar es Salaam mchana huu Juni 24, 2014. Kwa mujibu waliowahi eneo la tukio walisema kuwa dereva wa gari hilo alichanganywa na lori na kujikuta emeburuzwa mtaroni. Katika ajali hiyo hakuna aliyekufa ila dereva alikuwa katika hali mbaya na amekimbizwa hospitali ya Polisi Baracks.
Mashuhuda wakiangalia ajali huku mmoja wa ndugu wa aliyepata ajali akiangalia gari kwa mshangao.
Credit Kajunason Blog
No comments:
Post a Comment