Grace Loy (20), mkazi wa Mwananyamala Mchangani, aliyepigwa
risasi katika paja la kulia wakati wa vurugu iliyotokea.
MAMA mzazi wa binti aliyesababisha wasichana wawili
kujeruhiwa kwa kupigwa risasi na polisi baada ya kushiriki ngoma maarufu ya
Kanga Moko iliyopigwa marufuku, huko Mwananyamala Kisiwani jijini Dar es
Salaam, amefunguka na kusema kuwa hakukuwa na sherehe yoyote nyumbani kwake
siku hiyo ya tukio.
Mama huyo, Rehema
Aziz alisema waliojeruhiwa walikuwa wakisherehekea kuolewa kwa mwanaye aitwaye
Aziza Aziz, ambao walikuwa ni marafiki zake na walifanya hivyo kwa mujibu wa
mila za watu wa Pwani, za kucheza na kufurahi wakizunguka mitaani, lakini bila
kufanya fujo yoyote. “Huo ulikuwa ni Mdundiko wa kawaida, tokea zamani tulikuwa
hatuombi kibali na wao walifanya hivyo kama mila zinavyosema, siku ya tukio
Juni 18, mwaka huu hatukuwa na sherehe hapa nyumbani isipokuwa jana yake ndiyo
kulikuwa na sherehe ya kumpa zawadi mwanangu.
Majeruhi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Zawia Hamis
(20), mkazi Mwananyamala anayedai kupigwa risasi tumboni na kwenye makalio.
“Tukio la Juni 18,
wasichana ambao ni marafiki zake mwanangu ambaye kwa sasa yupo kwa mume wake,
walikuwa wakisherehekea wenyewe kivyao, bila mimi kujua, lakini
hata hivyo
mbona ilikuwa ni mapema mno, saa kumi jioni na walikuwa ni wanawake tu,”
alisema mama huyo.
Kwa upande wake majeruhi Grace Loy (20), mkazi wa
Mwananyamala Mchangani, alisema anachokijua ni kwa alipigwa risasi katika paja
la kulia wakati huo wa vurugu ya kuwataka watawanyike.
“Sisi tulikuwa tukiwasindikiza watu wa tarumbeta ambao
walikuwa wanaume, tuliobaki tulikuwa wanawake na hakukuwa na vurugu wala
hatukumpiga askari ila sisi tumepigwa risasi kama swala,” alisema Grace.
Majeruhi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Zawia Hamis
(20), mkazi Mwananyamala anayedai kupigwa risasi tumboni na kwenye makalio,
alisema ameshangazwa na kitendo hicho.
Walisema ni jambo la ajabu kuwa polisi walitumia nguvu kubwa
dhidi ya wanawake waliokuwa hawana silaha yoyote.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Makumbusho, Husna Nondo alisema
watu hao hawakuwa na kibali cha aina yoyote na kusisitiza kuwa serikali
imeshapiga marufuku ngoma za Kanga Moko hivyo amewataka wananchi kufuata agizo
hilo la serikali.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura
alipoulizwa juu ya suala hilo, alisema upelelezi unaendelea ili kubaini tatizo
No comments:
Post a Comment