Kutia alama mwilini umekuwa utamaduni kwa miongo kadhaa
katika maeneo tofauti barani Afrika ili kuashiria urithi wa kikabila.Vitendo
hivi hata hivyo vinapungua lakini bado kuna watu wanaotaka kuendeleza
kilichofanya na mababu zao.Katika mji wa Ouidah kaskazini mwa Benin, kuna
tambiko inayotarajiwa kufanyika ikifuatwa na siku mbili za sherehe.Houeda ni
mojawapo wa makabila nchini Benin inayoamini kuwa tendo la kuchanja watoto –
hasa usoni- huwaunganisha na mababu zao.
Watoto hao hupewa majina mapya, wananyolewa vichwa vyao na
kupelekwa katika makazi ya watawa ambapo kuna mizimu inayowasaidia kuzungumza
na vizazi vya hapo awali.
'Utamaduni unaoenziwa'
“Hii ni sehemu ya tamaduni zetu na ni muhimu sana kwangu,”
anasema Genevieve boko, ambaye mwanawe wa kike mwenye umri wa miezi 6, Marina,
pamoja na wapwa zake Luc na Hospice wenye umri wa miaka 10 na miaka 12 wote
wako tayari kuchanjwa.
Mpekuzi ilifanya mahojiano
na mama huyo
ambaye naye alionyesha
kushangazwa na tukio
hilo na kusema
hajui tatizo lililomfanya
ajifungue mtoto huyo
kwa kuwa hakuwahi
kusikia maumivu ya
aina yoyote wakati
wa ujauzito huo
hadi alipofikia hatua
ya kujifungua….
Katika mahojiano hayo, mama
huyo alisema kuwa
huo ni uzao
wake wa 6
na hajawahi hudhuria
Clinic
Jivu hutumika kutia alama sehemu ambayo chanjo hiyo hufanywa
na huchukua sekunde chache chanjo hiyo kufanya.
“Rafiki zangu waliniuliza iwapo ni uchungu na iwapo nililia
na nikasema ‘la!’,” alisema Luc baadae. “Kabla, nilipokuwa nikitembea mitaani
pamoja na ndugu yangu mkubwa aliye na makovu, watu hawangeamini kuwa ni ndugu
yangu. Sasa nina furaha kwa kuwa tunafanana.”Tangu mume wake alipoaga dunia,
Gamba Dahoui amekuwa akifanya chanjo zote za nyumbani-anasafisha vifaa vya
kuchanjia kwa mimea yenye dawa pamoja na tembo. Makaa pia huwekwa kwenye
majeraha ili kuyasaidia kupona.
Dahoui hutumia kisu kimoja tu kila wakati, huku akipuuza
mashari rasmi ya kutumia nyembe safi kwa kila mtu ili kuepuka hatari ya
kuambukiza magonjwa yanayoambukizwa kwa damu kama vile pepopunda na UKIMWI.Chanjo
hizi hata hivyo zimeanza kupoteza umaarufu. Idadi kubwa ya familia inashiriki
sehemu ya kwanza tu ya sherehe hizo, na kuacha kabla ya chanjo kufanywa.Ni sawa
sawa na sehemu mbalimbali ya taifa hilo ambapo kila kabila huwa na mfumo wake
wa kuchanja.
'Ni aibu kukosa alama au makovu'
“Nikiwa na makovu yangu, ninatambulika kila mahali ninapokwenda,”
anasema Fleury Yoro, anayeishi Atacora, kaskazini mwa taifa hilo. “Iwapo
ningepata nafasi ya kufanya uamuzi, singependa kuwekewa makovu namna hii.”
Anasema kuwa alipokuwa akisoma katika jiji kubwa zaidi
nchini Benin Cotonou, alikejeliwa mara kwa mara kutokana na makovu yake. Watu
kadhaa ‘‘hawangependa watu wengine wadhani kuwa walikuwa marafiki na mtu
mshenzi namna ile,” anasema.Wengine wana maoni tofauti ya kufanya uamuzi wa
kutochanja vizazi vichanga. Sinkeni Ntcha aliacha kitendo hicho baada ya watoto
wake 3 wa kwanza ‘‘kwa sababu ya UKIMWI,” anasema. ‘‘Nyembe zinapaswa
kubadilishwa kila wakati lakini wakuu walikataa.”Kwake, kama mmoja kati ya watu
wa kabila la Otomari, alama hizo “hazina maana”. Utamaduni unawezwa kuendelezwa
kwa njia nyingine, anasema, kupitia kwa lugha, densi, unyago na usanifu.Watu
wengi wa kabila la Otomari bado wanakubali kutiwa alama, wakiwemo wanawake
kadhaa wachanga ambao wakati mwingine huchanjwa kwenye migongo yao na tumboni
wanapobalekhe ili ‘‘kuonyesha ujasiri wako,” anasema Edith (aliyeonyeshwa
kwenye picha). Mifumo huwa sawa mara kwa mara na michoro inayochorwa kwenye
mijengo ya mitaani.
Wakati mwanawe Genevieve Boko, Marina (hapo chini) alipokuwa
na umri wa miezi 6 tu alipotiwa alama – watoto katika sehemu zingine nchini
Benin hufanyiwa kitendo hicho juma moja tu baada ya kuzaliwa.
Katika nchi jirani ya Nigeria, suala la haki za watu wachanga limesababisha baadhi ya majimbo kupiga marufuku zoezi hilo kwa watoto wote.
Katika nchi jirani ya Nigeria, suala la haki za watu wachanga limesababisha baadhi ya majimbo kupiga marufuku zoezi hilo kwa watoto wote.
Hata hivyo, hii sio hatua inayowapendeza watu wote wa Benin.
‘Hatukiuki haki za watoto, tunawaonyesha watoto walikotoka na kile
watakachopitia maishani,” anasema Telesphore Sekou Nassikou, mhariri mkuu wa
kituo kimoja cha redio mjini Natitingou iliyoko kaskazini magharibi mwa taifa
hilo.Kwake, makovu hayo hupitisha ujumbe: ‘‘Tahadhari, kuna uchungu katika
dunia hii, na utahisi uchungu katika maisha yako. Hata hivyo uchungu huo
utaisha iwapo utavumilia.”
No comments:
Post a Comment