Na Waandishi Wetu
HUKU watu karibia 60 nchini kenya wakiuawa kwenye
mashambulizi ya kigaidi, katika hali isiyo ya kawaida nchini Tanzania, walinzi
wa Maduka ya Mlimani City jijini Dar wamejikuta wakipata mchecheto wa aina yake
baada ya kitu kilichodhaniwa ni bomu kukutwa kwenye eneo la kuegeshea magari.
Walinzi wa maduka ya Mlimani City jijini Dar wakikagua kitu
kinachosadikika kuwa ni bomu.
Tukio hilo lilitokea Juni 16, mwaka huu ambapo kwa mujibu wa
shuhuda aliyeomba kusitiriwa jina, aliona gari dogo jeupe likiangusha kifaa
hicho kilichodhaniwa ni bomu kisha likatoweka.
Chanzo hicho kilizidi kudai kuwa baada ya gari kutoweka,
dada mmoja alipita eneo hilo na kukuta kitu hicho kilichofungwa nyaya kikiwa
ndani ya mfuko, akashtuka na kwenda kumtonya mlinzi wa eneo hilo ambaye alifika
mara moja na kuwaita wenzake.
...Ukaguzi ukiendelea.
Taarifa za uwepo wa kifaa hicho ziliwafikia waandishi wetu
waliokuwa wakipiga doria katika eneo hilo na haraka wakasogea karibu
kuwashuhudia walinzi hao wa Kampuni ya Ulinzi ya Omega wakiwa
wamekizunguka
kifaa hicho kwa umakini mkubwa.
Walinzi hao walimuita kiongozi wao ambaye alifika na
kukichunguza kifaa hicho ambapo alipokifungua aligundua ni betri bovu la
pikipiki.Waliichukua betri hiyo na kuitupa huku wakitawanyika kurudi kwenye
maeneo yao ya ulinzi.
Maoni ya Mhariri
Kutokana na kuwepo kwa matukio ya kigaidi yaliyotokea
nchini Kenya hivi karibuni, ni vyema jeshi la polisi likawa na
tahadhari katika maeneo yanayokusanya watu wengi kama Mlimani City.Chanzo GPL
No comments:
Post a Comment